GET /api/v0.1/hansard/entries/485511/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 485511,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/485511/?format=api",
    "text_counter": 89,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Kitu ambacho ni muhimu katika nchi hii ni usalama. Wakati mambo ya usalama yanachukuliwa kama mzaha, kila Mkenya anaona kwamba mambo hayaendi vizuri. Nilisikia mhe. mmoja akisema kwamba wakati mwingine unaitana na unaambiwa gari la polisi halina mafuta. Katika mwezi uliopita, kuna wakati niliuliza Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Usalama nchini kwamba--- Wakati mwingine tunasema tuna magari mengi sana yaliyopeanwa katika kila kituo cha polisi. Lakini ninataka kuuliza jambo moja; nilimwuliza OCPD kama hayo magari yamepeanwa kama maua ama ni ya kufanya kazi. Kama magari ni ya kufanya kazi, kwa nini useme kwamba una shida halafu isemekane kwamba gari halina mafuta? Kama gari limeletwa na ni la kufanya kazi, basi tuelezewe ni kwa nini halina mafuta. Kazi inakuwa ngumu, haswa katika maeneo ya uwakilishi Bungeni. Tunaona kwamba wananchi wanaumia, na hata wanauliwa. Lakini wakati wa kwenda kuwasaidia, unasikia kwamba kuna shida ya mafuta. Wakati mwingine hatuwezi kuelekeza kidole cha lawama---"
}