GET /api/v0.1/hansard/entries/485681/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 485681,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/485681/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Kwanza, ningetaka kumkosoa Mwenyekiti wetu kwa kusema kwamba kamati ziko katika lokesheni; hakuna kamati ambazo ziko katika lokesheni, bali ni mtu mmoja ambaye anasimamia Wadi. Mwanakamati ni mmoja katika kila wadi. Kwa hivyo, hata hii kazi ni ngumu kwa hao wanakamati kwa sababu ni wachache. Pili, ni lazima tuweze kuelezwa ni vipi ambavyo wataweza kuwasaidia hao wanakamati kwa sababu wengine wanatoka sehemu ambazo ziko mbali sana na ile ofisi kuu ambayo inasimamia mambo ya hizi pesa. Inawabidi wao kutumia pesa zao za mfukoni kuzunguka. Hakuna gari la serikali ambalo linawasaidia hawa watu wanapokua wakizunguka nyanjani ili kuweza kuwatambua watu hawa. Ukweli ni kwamba, pesa ambazo zinatolewa ni kidogo sana, inafaa ziongezwe, na hao wanakamati waweze pia kupatiwa kitu ambacho kitawasaidia katika usafiri wao. Ahsante Mhe. Naibu Spika."
}