GET /api/v0.1/hansard/entries/49040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 49040,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/49040/?format=api",
"text_counter": 387,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "ile. Wakati mwananchi wa Kenya anapopoteza maisha yake, awe ni wa kabila moja ama ingine, taifa nzima la Kenya linahusika. Katika nyakati kama hizo, tunastahili kuungana na kuzungumzia maisha ya Wakenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo la pili ni kwamba ni lazima tuielewe nchi yetu na nchi yetu ituelewe vilivyo, tukifahamu kwamba tumezingirwa na mataifa ambayo wakati mwingine, na kwa sababu fulani, hawana imani ama upendo na nchi yetu ya Kenya. Tumeweza kuhusika kwenye masuala ya mauaji ya Wakenya. Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani yuko hapa. Ni vigumu sana kujua mtu anayekuvizia atashambulia boma lako saa ngapi, na utamuzuia namna gani. Hata hivyo, ni jukumu la Serikali kuhakikisha kwamba jambo kama hilo likitokea kwa mara ya kwanza, halitokei tena. Kuna msemo wa Kiswahili unaosema: âKosa si kosa. Kosa ni kurudia kosaâ. Tumeona mataifa mengi ya kigeni, likiwemo taifa la Amerika, yakishambuliwa na kundi la kigaidi lililokuwa likuongozwa na Osama Bin Laden. Hiyo haimaanishi kwamba hakukuwa na ulinzi katika nchi ya Amerika. Lilikuwa jukumu la walinzi wa nchi hiyo kuhakisha kwamba mashambulizi kama hayo hayarudiwi tena. Kwa hivyo, yaliyotokea hivi karibuni, yemeshatokea. Tunamuomba Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani na mwenzake, Waziri wa Ulinzi, wahakikishe kwamba waweungana na kulinda maslahi ya Wakenya vilivyo."
}