GET /api/v0.1/hansard/entries/49043/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 49043,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/49043/?format=api",
"text_counter": 390,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa wale waliozungumza hapa na kuweka mipaka, wakisema kwamba tunazungumzia kabila fulani, ambako mauaji yalitokea, ningependa kusema kwamba sio watu walioko vijijini pekee wanaopoteza maisha yao. Hata Wabunge wanauawa kiholela. Wafanyikazi wa Serikali wanauawa kiholela. Wengine wanauawa wakiwa na walinzi wao. Maafisa wa polisi wenyewe wako hatarini ya kuuawa. Kwa hivyo, suala la mauaji na watu kuviziwa katika nchi siyo suala la Waziri peke yake, bali ni suala linaloihusu nchi nzima. Kama tunataka kuweka ulinzi katika taifa letu, ni lazima tuache kugombana kwa misingi ya kikabila na tuache kusema kwamba watu wa kabila fulani hawalindwi. Inafaa tuyaangalie mambo haya kwa ujumla, tukiweka akili zetu pamoja, na tuisaidie Wizara ya Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani, ili tunaposhuku kuweko kwa mpango wa kuchukua maisha ya Wakenya, hatua ichukuliwe mara moja dhidi ya mpango kama huo. Tusipofanya hivyo, tutakuwa tukiongea tu juu ya mauaji na mambo ya nchi nyingine. Bw. Naibu Spika wa Muda, haifai sisi kuonekana kana kwamba tunatuma ujumbe, kwa nchi jirani zetu, kwamba tunataka ugomvi na wao. Kenya iko katika ramani ya dunia, na haswa Africa nzima. Jambo hili limedhihirishwa katika siku zilizopita. Tusipochunga matamshi yetu, tutatoa dharau kwa nchi za nje, na hatuna uwezo wa kuzuia kupigwa kutoka kwa kila pembe. Kwa hivyo, kama mambo haya yametokea kutoka Serikali ya Ethiopia, ni lazima Kenya itume ujumbe kuzungumza na serikali ya nchi hiyo na kuafikiana kwamba haikubaliki wananchi wa Kenya kuviziwa na kuuliwa mara kwa mara."
}