GET /api/v0.1/hansard/entries/49044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 49044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/49044/?format=api",
    "text_counter": 391,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Hiyo ndiyo njia ya kidiplomasia tunayofaa kutumia kuzungumzia suala hili, na tutaheshimiwa. Hatutaki kuonekana na mataifa mageni kwamba tunaamka asubuhi na kutoa maneno ya dharau, tukionyesha kwamba tunaweza kupigana na mtu fulani. Anayechukua sheria mikononi na kupigana na jirani yake hatii hata sheria za Mwenyezi Mungu, bali anatumia uwezo wake mwenyewe na kuwadharau wanyonge. Kwa hivyo, tuchunge sana. Sisi tunatazamiwa kuiunganisha Afrika nzima, na ni lazima tusimame kwenye nafasi yetu. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}