GET /api/v0.1/hansard/entries/490967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 490967,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/490967/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza ningependa kumsifu Sen. Ongoro kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu. Ukiangalia kwa undani, utaona kwamba Hoja hii ina mambo muhimu sana. Ina mambo yanayohusu watoto ambao wanakuwa wazazi wakiwa na umri mdogo. Hili ni tatizo ambalo sisi kama viongozi ni lazima tulivalie njuga. Lakini kwanza, tutafute sababu. Tukubaliane ya kwamba hivi sasa mazingira yamebadilika na sio yale ya zamani. Huu ndio ukweli wa maneno. Mfumo wa digital na dot-com unaleta haya. Hivi sasa kuna simu na mitandao. Wanafunzi wanafahamu kila jambo. Kuna kitu kinachoitwa Facebook. Pia kuna kitu kinaitwa WhatsApp . Haya ndio mambo ambayo yanaleta madhara haya. Maendeleo huja na madhara yake. Hapa kuna mambo mawili; kuna watoto wa shule kwa watoto wa shule. Hili ni jambo ambalo ni lazima tulikemee kabla ya kutafuta suluhisho. Pili, kuna watoto wa shule ambao wanapata uja uzito na akina baba, ilhali wanajua vizuri kwamba wale ni watoto wa shule. Kazi ya akina baba hawa ni kufuata watoto wa shule na kuwadanganya hapa na pale. Hii ni hatari. Siku hizi watoto wa miaka 12 wamenona na kujaza kila mahali. Utafikiri kwamba ni mtu wa miaka 20 kumbe ni mtoto. Hii ni kwa sababu ya kula vizuri. Ni lazima tuhakikishe kwamba akina baba kama wale hawaruhusiwi hata kidogo kucheza na watoto wa shule. Bw. Naibu Spika, pia tunafaa kukubaliana kwamba tabia za wazazi wengine sio nzuri. Wewe una mtoto wako lakini una mpenzi huyu, mara yule mwingine. Je, mtoto atafuata tabia gani? Ataona kwamba labda kuna mambo mazuri pale. Kwa hivyo, sisi wenyewe kama wazazi ni lazima tuzingatie mambo fulani. Tunajua kwamba maendeleo yana taabu. Tangu enzi ya televisheni kufika, wengine wetu tumeacha mila zetu za Kiafrika na kuwa kama wazungu. Hii imetuharibia. Wengine wetu tunavaa suti na kufunga tai kama wazungu wa London. Tunataka mambo ya kizungu. Kwa kuwacha mila zetu za Kiafrika, ule mwongozo wa zamani uliokuwa ukitumiwa kulea watoto umepotea. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}