GET /api/v0.1/hansard/entries/490969/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 490969,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/490969/?format=api",
    "text_counter": 93,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hivyo, tunafaa kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba watoto wanaopata watoto wanaangaziwa. Pia, tunafaa kuweka mikakati ya kuzuia mambo haya. Hii ni kwa sababu kuna watu ambao wanaweza kutafuta mwanya. Akijua kwamba mtoto akipata mimba atalelewa na Serikali, nia yake itakuwa kuwapachika watoto mimba. Kama kutakuwa na hatari ya kufanya kitu kama hicho itakuwa vizuri. Yule anayefanya kitendo kile hafai kuachiliwa huru. Ni lazima tuyatilie mkazo mambo hayo. Bw. Naibu Spika, dini zote zikiwemo Waislamu na Wakristo zinafaa kutilia jambo hili mkazo ili kuhakikisha kwamba watoto wetu wanapata elimu ya dini. Hii itawaondoa kwa haraka ya kupapia maisha. Hii haraka ndio inaleta madhara haya. Waswahili husema: “Mramba asali harambi mara moja, maanake anasikia utamu.” Sasa hii ndio hatari ambayo iko hapa. Ni lazima tuhakikishe kwamba watoto hawakimbilii hiyo asali. Asali hii ambayo wanataka kulamba haraka haraka ndio inaleta madhara haya. Kwa hivyo, tunafaa kutilia mkazo mambo ya dini. Watoto wetu wanafaa kufundishwe maadili ambayo ni sawa. Bw. Naibu Spika, pia siku hizi mwanafunzi akiadhibiwa na mwalimu ni balaa. Wanafunzi hivi sasa wanaweza kuwaeleza walimu kitu cha kufanya. Tumewapatia uhuru mwingi sana ikilinganishwa na zama zile. Mwalimu alikuwa mwelekezi wa mwanafunzi, lakini hivi sasa mtoto wako akiadhibiwa, wewe unakuwa mtu wa kwanza kufika shuleni na kulalamika. Bw. Naibu Spika, naunga mkono Hoja hii kwamba kuna haja ya watoto hawa kurudi shule baada ya kujifungua. Pia, kuna haja ya kuweka mikakati iliyo na tahadhari. Kuna watu wanaoweza kutumia mwanya kuhakikisha kwamba mambo hayaendi vizuri. Bw. Naibu Spika, kuna vipindi vingi kwenye televisheni. Kuna kipindi kama"
}