GET /api/v0.1/hansard/entries/490971/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 490971,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/490971/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kipindi hiki ni cha kutafuta wapenzi. Sasa mwanafunzi anatafuta mpenzi. Je, ni nini kinatafutwa hapa kama sio mimba? Haya ni mambo hatari na huu ni ukweli ambao lazima usemwe. Mtoto akitoka shule anaangalia vipindi hivi kwenye televisheni. Hii inachangia kuenea kwa mambo haya. Mimi sishutumu kipindi cha Tujuane lakini ni lazima mambo haya yafanywe kwa mpango. Ni lazima tujue ni mambo gani yanadhuru umri gani. Tukiwacha hali iendelee, basi tujitayarishe kuwa na wazazi wengi ambao ni watoto. Jambo hili ni lazima litiliwe mkazo. Bw. Naibu Spika, naunga mkono pendekezo kwamba pesa ni lazima zitengwe ili kushugulikia jambo hili. Bw. Naibu Spika, kwa hayo mengi, naunga mkono Hoja hii na kumpongeza Sen. Ongoro."
}