GET /api/v0.1/hansard/entries/490998/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 490998,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/490998/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Hoja hii. Bw. Spika wa Muda, kwanza nampa hongera dada yetu, Sen. Elizabeth Ongoro, kwa kuleta Hoja hii. Jambo la kwanza la kuzingatia kama Wakenya ni kwamba familia ni msingi mkubwa sana wa maendeleo. Biblia inasema kwamba familia inayoomba pamoja inaishi vyema kwa muda mrefu. Ukiwa na familia ni lazima uwaelimishe watoto wako kama kiongozi ama mama wa familia. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii kwa sababu wengi wa vijana wetu hivi sasa katika sehemu mbalimbali, hasa Kilifi kule ninatoka wameingilia mambo ya mihadarati. Watu wanapitia njia za vichochoro vya nchi kavu au kando kando ya bahari na kuleta mihadarati mbalimbali. Mihadarati hii inaleta madhara makubwa kwa watoto wetu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}