GET /api/v0.1/hansard/entries/491000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 491000,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491000/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nachukua nafasi hii pia kumpongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kazi aliyoifanya katika Bahari ya Hindi. Sisi wakaazi wa Pwani na watu wote wa Kenya kwa jumla walimuona akienda kule Bahari ya Hindi. Kulikuwa na meli ambayo ilikuwa imeshikwa kwa kupatikana na mihadarati yenye thamani ya zaidi ya bilioni moja. Hii ni mihadarati ambayo ingeharibu au kuua kizazi kizima cha vijana wetu. Waswahili husema, “Mgala muuwe lakini haki yake pia umpatie.” Alichofanya Rais ni kitendo ambacho kiliokoa maisha ya vijana wetu katika Kenya. Bw. Spika wa Muda, akina mama wetu wanafaa kuwafunza watoto wao, hasa wale wa kike maadili mema. Ni rahisi sana kwa mtoto wa kike kuharibika akiwa mdogo. Akina mama wetu wanafaa kuwajibika. Ni lazima waelimishe watoto wao wa kike na wa kiume kuhusu madhara ya kujihusisha na mambo ambayo hayafai kama utumizi wa mihadarati. Bw. Spika wa Muda, pia katika jamii zingine kuna wazee ambao wanaoa watoto wa hata miaka minane. Wanaishi nao mpaka watakapofika miaka 11 ama 12 na kuanza kufanya mapenzi nao. Tabia kama hizi za kuoza watoto wetu wa kike mapema zimekithiri sana katika taifa letu la Kenya. Ni lazima tuwe na njia za kuandaa mabaraza ili wazee wetu waweze kuelezwa kwamba vitendo kama hivyo haviwezi kuendeleza taifa letu. Pia kuna wazee ambao hawana adabu. Wanaishi na watoto ndani ya nyumba kisha kulala na watoto wao wa kike. Tunafaa kutunga sheria ya kuangazia mambo kama hayo pia. Hatua kali inafaa kuchukuliwa dhidi ya wazee wenye tabia kama hizo. Bw. Spika wa Muda, vijana wetu ndio msingi wa maisha yetu ya kesho. Ukitembelea nchi za Ulaya utaona ya kwamba wazee ndio wengi. Hivi sasa watu wanalipwa kuzaa katika mataifa ya ulaya. Lakini sisi tunazaa zaidi na wazee wetu ni wachache. Lakini ili taifa liwe na uchumi bora ni lazima liwe na vijana wenye elimu nzuri. Ni lazima wajiepushe na njia mbaya ili kesho yetu ya Kenya iwe bora. Bw. Spika wa Muda, pia nataka kuzingatia sana Wizara ya Elimu. Wizara hii inafaa kuanzisha taratibu za kuwafundisha watoto wachanga, hasa kuhusu kujiepusha na mambo ya kufanya mapenzi wakiwa bado wachanga. Jambo la kushangaza ni kwamba unaweza kupata mtoto wa miaka kumi ambaye anajua mambo ya tarakilishi na mitandao. Wakati baba anaangalia televisheni, mtoto anaangalia mambo ya mapenzi katika simu yake ama tarakilishi kwa sababu ako na uwezo wa kuingia ndani ya mtandao. Jambo kama hili ni la kusikitisha kwa sababu linazorotesha uwezo kwa kujua vile Kenya yetu ya kesho itakuwa, hasa watoto wetu wakianza kujihusisha na mambo ya ngono wakiwa wadogo. Bw. Spika wa Muda, pia makosa yako katika mipangilio yetu katika Serikali. Serikali yoyote ambayo inahitaji kuwa na maendeleo zaidi ni lazima iwe na mipangilio ya kuona kwamba vijana wanaomaliza masomo katika vyuo vikuu au polytechnic wanapata kazi. Vijana wengi hasa wasichana wanapomaliza masomo hawapati kazi. Inakuwa rahisi sasa kwa mtu kama yule kuwa “chuo” cha shetani. Wanajihusisha na mambo ambayo hayafai. Kwa hivyo, Hoja hii ni muhimu kwa nchi yetu ya Kenya. Ni lazima tuwe na mikakati ya kuweza kuzindua njia za kuhakikisha kwamba vijana wetu wanapata kazi punde tu wanapomaliza masomo yao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}