GET /api/v0.1/hansard/entries/491303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 491303,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491303/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mimi pia ni mmoja wa Wanakamati wa Kamati hii nzuri ambayo imeleta Ripoti hii iliyoko mbele yetu leo na tunayoijadili kama Hoja. Bi. Spika wa Muda, ukweli wa mambo ni kwamba tulizunguka kaunti nyingi katika nchi hii; na katika mzunguko ambao Kamati ilizunguka, tuliona kwamba Kenya ina rasilmali nyingi sana. Katika kila kaunti tuliyopata fursa kuitembelea, tuliona kwamba rasilmali ziko na zimekuweko, na zitaendelea kuweko. Kwa hivyo, mjadala wa kwamba Kenya iko na rasilmali au la, jambo hili halina tashwishi wala shaka. Shida, mtihani bin examination ilikuwa je, kutokana na rasilmali zile, je, yule mwananchi wa kawaida anafaidika vipi? Huu ndio uliokuwa mjadala mkubwa. Mambo ambayo tuliyakuta na kuyaona ni kwamba wale ambao waliokuwa na matumbo makubwa walizidi kunona; mashavu yalizidi kuwa makubwa na meupe; ilhali watu wa kule walikuwa wanazidi kukonda na kuwa wembamba. Huu umekuwa ni mtihani na tulikuwa na mshangao mkubwa! Bi. Spika wa Muda, tulipokwenda Kaunti ya Machakos, tuliona watu wamezidi kuwa wembamba ilhali wauzaji michanga wanazidi kunona, huku wakizunguka na magari makubwa – Fuso ambazo zinauza mchanga hapa Nairobi. Lakini watu wa Machakos hali yao ilikuwa taabani kwa njaa; imekuwa hatari bin danger! Isitoshe, tulienda Kajiado na tulipofika huko, kulikuwa na mradi ambao ulikuwa unatengeza kokoto. Kampuni kubwa ya China ilikuwa imepewa mradi huu ambapo rasilmali ya kokoto iliyokuwa inatumiwa kujenga barabara za bypass ilikuwa inatengezwa. Lakini ukiwaangalia watu wenyewe wa Kajiado, shuka zao ni zile zile nyekundu; hawana dalili ya kuwa na manufaa yoyote. Tulipowauliza “Je, kaunti ya huko inapata chochote?” Ilikuwa ni masikitiko; tulitokwa na machozi. Mwenyekiti wetu alikuwa karibu kutokwa machozi lakini nikampa kitambaa cha kuvuta machozi; Naibu Mwenyekiti, Sen. Wamatangi, alikuwa yualia kwa huzuni iliyotupata kule. Huo ndio ukweli wa maneno. Bi. Spika wa Muda, kutoka hapo, tulienenda hadi Kaunti ya Baringo ambapo tulikuta geothermal energy . Tumesifiwa kwamba umeme wa megawati nyingi zitakazosambazwa katika nchi; lakini tukitizama hali ya watu wa Baringo, hali zao zilikuwa taabani! Huu ndio mjadala mkuu. Tulipofika Murang’a, tuliambiwa jinsi gani watu wa Nairobi wanaoga kwa maji ambayo yanatoka Bwawa la Ndakaini – sisi pia tukiwa katika kati ya hao wenye kuoga na maji yanayotoka kule. Swali ni: Je, watu wa kule wanapata nini kutoka kwa maji yale? Hamna kitu wanachopata! Lakini sisi watu wa Nairobi, sote twaoga kwa maji yanayotoka huko; tena sasa ndio twang’ara zaidi kwa sababu ya maji ya kutoka huko. Tulipofika katika mradi huo, tulipouliza kaunti ya huko yapata nini, tuliambiwa kuwa hii ni rasilmali ya kitaifa. Bi. Spika wa Muda, kutoka huko, tuliabiri hadi Kaunti ya Kwale – sikujui huko ni wapi – huko ndio mtihani bin danger! Huko Kwale, tulikuta rasilmali nyingi; kulikuwa na mradi wa base titanium; kulikuwa na mradi sijui wa Cotec ; kulikuwa pia na mradi wa"
}