GET /api/v0.1/hansard/entries/491309/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 491309,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491309/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi. Spika wa Muda, mambo mengine ni hatari bin danger. Hayo ndio mambo tuliyoyakuta yakiendelea kila mahali. Hili ni jambo linaloweza kuleta taswira mbaya, na ndio maana twasema kuwa Hoja iliyoko mbele ya Seneti hii na ule Mswada utakaokuja kujadiliwa na Maseneta kusudi tuhakikishe kwamba mambo yale yamezingatiwa huko mashinani kwa sababu ni muhimu. Sisi sio wa kwanza kuwa na rasilmali. Nakubaliana na wenzangu wengi waliosema kwamba kuna nchi ambazo zimeendelea kama Norway na nchi nyingine nyingi. Kuna nchi kama Tanzania ambayo imekuwa na mambo kama haya; wamekuwa na rasilmali lakini kila siku utaona ya kwamba vita vikubwa vinasababishwa na rasilmali. Hata sisi wenyewe tulipigana mpaka tukaleta mabadiliko ya Katiba na hii ni kwa sababu ya ung’ang’anizi huu. Na bado twasema ya kwamba tuna haja, sisi kama viongozi, kuhakikisha kwamba rasilmali zinawafikia wananchi wa kawaida, kwa sababu mwananchi yule wa kawaida ndio mtu muhimu. Ndio maana mimi naisifu Kamati hii The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}