GET /api/v0.1/hansard/entries/491311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 491311,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491311/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kwa kazi nzuri iliyoifanya katika ugavi, katika maono na kando ya kuja na Hoja hii, pia kuja na Mswada ambao utakuwa wa kisheria kueleza namna gani rasilmali zitagawanywa, namna gani kila kaunti itaweza kupata mgao wao pamoja na wale watu wanaokaa karibu na hapo kusudi faida ya rasilmali hizi iweze kumfikia yule ambaye yuko karibu na rasilmali zile. Kutokana na fikra zilizoko kwa wengi ni kwamba huko Afrika ni watu wa kunyanyaswa kila siku tu; tuwe exploited. Kama alivyosema Sen. (Dr.) Khalwale, wengine watafikiria matumbo yao tu; wengine watafikiria namna gani watawanyanyasa watu wao. Lakini la msingi ni kuona vipi watu wetu wa kawaida – kina Wanjiku, Fatuma, Wairimu, Kipkemboi na wengine – waliopo kule mashinani watakavyofaidika na swala hili. Kwa hayo mengi na machache, Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Asante, Spika wa Muda."
}