GET /api/v0.1/hansard/entries/491317/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 491317,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491317/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo nakumbuka ililetwa kwenye Seneti tukiwa na vikao vyetu kule KICC na niliweza kuichangia vilivyo. Ninashukuru kwamba Ripoti hii imeletwa hapa ili niweze kuichangia kikamilifu. Ni dhahiri shahiri kwamba tuliponyakua Uhuru wetu walioongoza taifa letu wakati huo na wale viongozi wa hivi sasa, wamesahau kwamba hatukupiginia Uhuru ili tupate viti ama uongozi wa kisiasa na nafasi katika vitengo vingine vya Serikali huku tukisahau kwamba urithi wa taifa letu upo ndani ya rasilmali zetu. Ninasema hayo kwa sababu katika taifa letu, wale walioko katika uongozi wanapiga siasa kuanzia asubuhi hadi jioni. Vile vile, wale ambao hawako uongozini wanapiga siasa kutoka asubuhi hadi jioni hasa wale ambao hawana kazi. Tumekosa mwongozo wa kuzungumzia watu wetu kama viongozi na kuwaambia kwamba matumaini ya maisha mema hayako katika ulingo wa siasa peke yake, ila katika rasilmali zetu. Bi. Spika wa Muda, mimi nimekuwa mchimba madini kwa miaka mingi sana na nimeweza kutembelea nchi mbali mbali. Nimetembelea nchi kadhaa za Amerika Kusini, Bara la Afrika na Asia, na nimeona vile rasilmali zinatumika. Ni jambo la kusitkitisha sana ukiangalia Kaunti ya Machakos. Nimefurahi sana kwamba Kamati hii iliweza kufika Machakos na kukutana na viongozi wake. Yale yote ambayo yamesemekana hapa ni mengi. Lakini ningependa kusema kwamba changarawe asili mia 70 iliojenga Mji wa Nairobi ilitoka Kaunti ya Machakos. Mapato ya watu wa Machakos ni mito yao. Hilo ndilo tegemeo lao la maisha. Mapato yanayopatikana kule Machakos ni duni mno. Wale wanaouza changarawe kule Machakos ni maskini wa kupindukia. Watoto wao wanaishi katika hali ya upweke ilhali kasheshe ilioko kule nia yake ni kuharibu tegemeo la watu wa Machakos. Wanaotoa changarawe na kuuza hapa Nairobi wanapata mamilioni ya pesa lakini ajabu ni kwamba Serikali ambayo ingelinda maslahi ya wananchi inawatoza pesa za kupata leseni kwa miezi mitatu. Kwa hiyo miezi tatu ni zaidi ya magari 180 ambayo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}