GET /api/v0.1/hansard/entries/491319/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 491319,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491319/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "yatachukua changarawe na wanapouza hapa Nairobi, unatambua kwamba wale watu wanaibiwa. Hata Serikali ya Kaunti ya Machakos ilitoa leseni ili mito hiyo iendelee kuharibiwa bila kuangalia kwamba pesa zinazolipwa zinaweza kuwafaa wananchi. Bi. Spika wa Muda, changarawe inachanganywa na posalana na madini mengine kutengeneza simiti. Kilo 50 za simiti zinauzwa kwa Ksh750 kwa kilo huku kilo 1,000 za mchanga wa changarawe inauzwa kwa bei duni. Kwa hivyo, tunapoongea mambo haya, haimaanishi tunamlenga mtu fulani. Katika kila pembe ya taifa letu kuna rasilmali aina tofauti. Kwa hivyo, ni juu yetu kuzingatia na kuunga mkono Hoja hii ili watu wetu wasaidike. Kaunti ya Machakos ina mabwawa matatu ya kutoa maji; Masinga, Kiambere na Kindaruma. Ninajua kila mtu kwenye Bunge hili analipia stima. Tunajua zile pesa tunatoa ili tulipe stima, lakini tunasikitika kwa sababu ukienda Kaunti ya Machakos ambako tuna mabwawa haya halafu utembelee--- Kuna kampuni inayoitwa KenGen ambayo iliteka mashirika ambayo yalikuwa ya Serikali bila kutoa hela hata kidogo na imekuwa mali yao. KenGen wanachukua ile stima bila kufanya chochote halafu wanaungana na Kenya Power Company na kutuuzia stima ilhali yule mwananchi wa Machakos Kaunti, isipokuwa kufukuzwa ili asikaribie lile bwawa, hapati chochote. Ukiangalia idadi ya magari ya KenGen, inaonyesha kwamba ni Shirika la Taifa la Kenya, lakini kwa undani, Serikali ya Kenya ina hisa duni mno katika hiyo kampuni. Hiyo ni kampuni ya kibinafsi ilhali imepakwa sura ya kuonyesha kwamba taifa la Kenya ni mshiriki katika ile kampuni. Kwa hivyo, wale wananchi hawagusi yale maji wala kuyanywa. Ningependa kuiambia Seneti hii kwamba ukienda katika Bwawa la Masinga, utakuta wananchi ambao wanaishi mita 300 ambao hawayanywi maji hayo. Mwananchi yeyote akiyanywa maji hayo, atajipata jela. Tuna Serikali ambayo inafaa kuwasaidia wananchi wa Kenya. Mswada huu utakapokuja hapa, nitapendekeza mabadiliko katika vipengele fulani. Ni juzi tu ambapo nilizungumza kuhusu mito yetu katika nchi hii. Niliileta Hoja na ikapitishwa. Bi. Spika wa Muda, huko Mavoko, Athi River, makampuni yanayotengeza vitu katika viwanda humwaga uchafu wao katika mito Tana na Athi. Mito hiyo ni rasilmali. Sisi huenda kukopa pesa ulaya ili tuchimbe maji tukiwa na maji ambayo yanaharibiwa. Leo nimejua kwamba kokoto ambayo inatumika kujenga nyumba hapa Nairobi hutoka Machakos. Huo ni ukweli lakini sio wote. Kabla kokoto kupatikana, mawe ya kujenga huwa kwanza lazima yapatikane. Mawe hayo huchongwa huko Machakos na kuletwa jijini Nairobi ili kutumika kujenga. Wenye mashamba na sehemu ambazo hutoka mawe hawapati kitu. Kokoto na mawe huchimbwa na kutolewa. Tunazungumuza mambo ya rasilmali. Nina ujuzi katika sekta ya madini. Tumewasomesha watoto wa watu ambao wamesomea Geology. Geologists wanapiga viatu rangi hapa Nairobi ingawa wanaujuzi wa utafiti wa kuyatafuta mawe. Ukienda katika uchimbaji wa madini, utashangaa sana. Utapata kwamba wanaoitwa wachimbaji wadogo wa mawe ni wale ambao wanalipa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}