GET /api/v0.1/hansard/entries/491970/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 491970,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491970/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, tunapoenda kutatua haya matatizo, ninatumai kwamba Ofisi ya Spika imemtengea kila Seneta jukumu lake na kazi atakayoitekeleza kwa wakati huo. Tunajua kwamba kuna Kamati ambazo zinahusika, lakini kuna kazi za ziada ambazo wengine wetu katika Seneti hii tutapewa kutekeleza. Palipo wazee hapaharibiki jambo. Kipengele cha 19 cha Katiba kinaeleza kinagaubaga kwamba iwapo matatizo kama yale ya Makueni yataendelea, basi tume itaundwa na Rais wa nchi. Tume hiyo itaangalia matatizo hayo kisha Rais anaweza kuivunja serikali hiyo ya kaunti ambayo imeshindwa kutekeleza wajibu wake na uchaguzi ufuate baada ya siku 90. Sisi kama Seneti hatutaki kwenda kuwazuia Wabunge wa kaunti hizo kutekeleza wajibu wao. Wanawajibu wa kufanya impeachment. Hilo silo jukumu letu. Hata kama kaunti zote 47 zitajitokeza na kuleta maombi ya kuvunja serikali zao, huo sio wajibu wetu. Tutasikiliza na kuamua. Lakini iwapo sasa maisha ya binadamu yako hatarini na watu wanatumia bunduki kushoto na kulia, nafikiri kuwa tunajukumu kama viongozi wa nchi hii na Seneti la kwenda mashinani ili kusuluhisha matatizo, kuleta uwiano na labda kupunguza uhasama na kupotea kwa pesa za serikali hizo. Kazi ya serikali hizo sasa ni kwenda kortini na kutumia pesa. Bw. Spika wa Muda, tukiwa na wajibu huo tuna shida moja ambayo ni mahakama. Je, tutafanya nini? Tukienda kule mashinani tutakuja na uamuzi na stakabadhi ambazo tutawasilisha kwa Seneti hii. Lakini mahakama imekuwa janga na chuma katika ubongo wa Seneti. Wameamua kuharibu serikali za kaunti. Wanataka kuvunja ugatuzi. Seneti inafaa kupeleka kilio chao kuhusu mahakama kwa wananchi wote. Mahakama zimevunja ugatuzi. Wananchi wamenusa maendeleo kwa sababu pesa zimepelekwa hadi mashinani kupitia ugatuzi. Hata hivyo mahakama imeharibu jambo hili. Je, wanamtendea kazi nani? Je, wanamtukuza nani na lengo lao ni nini? Je, sababu zao za kufanya hivyo ni nini na watapata faida gani? Maswali haya ni lazima yajibiwe, kwa sababu nafikiri kwamba mizizi ni mirefu. Sisi tunaona matawi tu. Je, mizizi yake iko wapi? Bw. Spika wa Muda, naunga mkono."
}