GET /api/v0.1/hansard/entries/491972/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 491972,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/491972/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "October 2, 2014 SENATE DEBATES 29 Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii ili tuweze kwenda nje na kutafuta suluhu katika Kaunti za Makueni na Isiolo. Tulipokuwa na utata katika Kaunti ya Machakos, Korti pale Machakos ilitoa uamuzi wa kusimamisha Bunge la kaunti hiyo kufanya kazi yake. Ilitoa uamuzi kwamba kazi ingefanyika kulingana na sheria na Katiba ya nchi hii. Baadaye tuliunda Kamati Maalum ambayo ilikaa na kufanya kazi kulingana na Katiba. Licha ya kuwa Kamati yetu ilikubaliana na Bunge la Kaunti ya Machakos, Seneti hii ilitumia Katiba hiyo hiyo kuamua kwamba maneno hayo hayakuwa sawa. Kwa kauli moja, tulikubaliana na maneno hayo yakakoma. Bw. Spika wa Muda, kuhusu mambo ya Kaunti ya Embu, mahakama iliingilia mambo haya kutoka mwanzo. Katiba inaruhusu Bunge la Kaunti ya Embu kuzungumzia Hoja kuhusu Gavana wa Embu. Katiba pia inasema kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu jambo hili si wa bunge la kaunti wala ni wa Seneti. Korti tena ilitoa uamuzi mambo yasifanyike. Tulikuwa huku hatukuwa na habari, tulikuwa tunafanya kazi yetu halafu tukaona maamuzi ya korti yakija yakisema kuwa Bunge La Seneti limedharau mahakama, limeendelea na kazi ya kumshugulikia Gavana wa Embu. Hoja ilirudishwa mara ya pili lakini mahakama tena ikaingilia mambo haya, ikaleta sarakasi na kasheshe. Mpaka wa leo, ukamilifu wa mambo ya Gavana wa Embu hayajulikani kama ni Korti, Seneti, Bunge ya kaunti ya Embu ama ni wananchi walio na mwisho wa mambo haya. Bw. Spika wa Muda ningetaka kujulisha Seneti hii kwamba katika mkutano wetu wa Kamati ya Rules and Business unaofanyika Jumanne, Mhesihimiwa Spika aligusia kwamba tarehe 23, 24 na 25 Oktoba, tutafanya mkutano wa faragha na kuweza kuzungumza yanayohusu Bunge hili na mahakama. Ni dhahiri kwamba Seneti ikubaliwe ifanye kazi yake kulingana na Katiba au ifutiliwe mbali, tuwache kufanya kazi ya bure. Kuna haja gani sisi kukaa hapa na kufanya kazi masaa mane or sita, kama ile kazi tulifanya ya kupitisha Hoja iliyoletwa hapa kuhusu Kaunti ya Embu na mwishowe tunaanza mlolongo wa maneno mpaka mwisho haujulikani. Ukiangalia mambo yanayohusu Kaunti ya Makueni, na tumejaribu kama vile ndugu yangu Seneta Musila amesema, shida ya Makueni ni uongozi na tama ya pesa pekee yake. Hakuna mambo mengine. Gavana ana simama na kusema: “Sheria inasema tutumie pesa mpaka hapa.” Wengine wanasema: “Hapana, Kaunti za Nakuru, Machakos na Meru zinatumia pesa hivi ama vile.” Ningetaka ndugu zangu hapa wajue mambo haya. Vita sio baina ya watu wawili. Waliopigwa risasi kule Makueni ni wa upande mmoja, wale ni watu wa Gavana. Hakuna risasi iliyotoka upande wa Gavana kumpiga mwingine wa upande ule mwingine. Kwa hivyo, wanao hamaki kwa roho zao na mambo haya ni wale ambo wanasingizia mambo ambayo Seneti inakataa. Bw. Spika wa Muda, tunahitaji muda kuangalia mambo haya. Kwa hayo, machache, ninaunga Hoja hii mkono."
}