GET /api/v0.1/hansard/entries/492150/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492150,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492150/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "umma, huduma ambayo ni nzuri, huduma ambayo haitaumiza watu, huduma ambayo ni rahisi na itarahisisha usafiri. Vijana ambao wanashughulika na kazi ya boda boda mara nyingi wana shida. Moja ya shida wanazokumbana nazo ni ukosefu wa mafunzo ya kutosha. Kama wangekuwa wamefunzwa uwajibikaji, na kujua sheria za barabarani kulingana na sheria za usafiri, bila shaka, ajali tunazoziona nchini mwetu zingekuwa zimepungua. Jambo lingine ni kuhusu vifaa. Utakubaliana nami kuwa mara nyingi hawa vijana wanabebana bila kuvaa kofia ambazo zinaweza kuwasaidia wakati wa ajali. Abiria ambao pia wanabebwa nao hawawezi kuvaa hizo kofia. Hawana nguo ambazo zinaweza kuonyesha mtu usiku kuwa hapo mbele kuna boda boda. Mara nyingi ukosefu wa vifaa unachangia kuweko kwa ajali. Kuna sehemu nyingine za nchi ambapo unaweza kwenda hospitalini ukakuta pahali pametengwa pa watu ambao wamepata ajali ambazo zimetokana na boda boda. Hiyo haimaanishi kuwa biashara si nzuri. Inaweza kuboreshwa na tunaomba serikali ije na shughuli mwafaka za kuweza kuboresha sekta hii ya boda boda. Mna kitu ambacho kinaendelea inchini mwetu kuhusu hawa vijana wetu wa boda boda na polisi. Polisi ambao wamejitoa badala ya kuangalia wezi huko mitaani, wamekuwa ni kuamka asubuhi na kujipanga kwa barabara ili kuwanyanyasa hawa vijana. Unaweza kuona kuwa kijana amesafirisha, na kupewa Kshs.200 ama Kshs.300 akikutana na polisi bila shaka hakuna kosa litakalo patikana katika gari lake la usafiri. Mara nyingi utakuta analazimishwa atoe hongo kwa polisi; polisi hua hawana haya kuona kijana amerauka asubuhi, amepigwa na baridi angalau ajitafutie ajira, na hizo fedha kidogo amepata, kama Kshs200 pia wanamnyanganya. Kuna mambo mengi tumeyashuhudia hata katika sehemu ambayo nawakilisha, Wundanyi. Utakuta boda boda zinazotoka Mgange kwenda Mgange-Dawida, polisi wamejipanga njiani kuwanyang’anya hawa vijana pesa. Wundanyi kwenda Wesu ni hivo hivo; Viruga kwenda Wesu, hivo hivo, Viruga kwenda Mgambonyi ni hivo hivo. Kwa hivyo, tunawaomba polisi nao watusaidie kuboresha sekta hii badala ya kuwa tayari kila wakati kuwanyanyasa hawa vijana. Serikali pia ingetoa hundi kuwasaidia hawa vijana. Hawa vijana mara nyingi wanaendesha magari njiani ambayo mara nyingi si yao; hua kuna watu ambao wameyanunua na wakawaajiri vijana ili jioni angalau wajipatie riziki zao. Sasa hawa vijana wataendesha hizi boda boda mpaka lini? Tunatarajia nao pia watapata nafasi ya kuweza kuinuka kimaisha, na kutoka katika hiyo sekta ya boda boda, na kununua magari kama matatu ; lakini wanaanza chini na boda boda. Litakuwa ni jambo la busara kwamba kwa vile Serikali ilitenga hela ama fedha za akina mama na vijana sasa ifikirie kama inaweza kutenga hela za vijana wa boda boda. Bunge hili lina mamlaka ya kuweza kutoa pesa ambazo zinaweza kutumiwa kuwafadhili vijana ambao wanashughulika katika sekta hii ya boda boda ili iweze kuboreshwa. Hizi pesa za CDF ambazo tunazitumia, wengine wetu tumezitumia kuhakikisha kuwa vijana wamepata mafunzo, wameelimishwa kuhusu uendeshaji magari na boda boda. Lakini haitoshi. Mara nyingi fedha tulizo nazo ni chache na hazitoshi. Litakuwa jambo la busara Bunge lifikirie kukaa chini na kuona kama tunaweza kuweka kiwango fulani katika kila eneo bunge ambacho kitatumiwa kuwafadhili hao vijana; fedha hizo zitatosha kuwapatia mafunzo na hata mikopo ya kunua pikipiki ili wazitumie kufanya biashara yao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}