GET /api/v0.1/hansard/entries/492152/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492152,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492152/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Nakushukuru Mhe. Spika. Mjadala uliopo mbele yetu, kwa maoni yangu, ungekuwa imefanyika mwaka jana. Hata hivyo, ni shukrani maanake leo tumepata kuujadili. Hoja hii ni muhimu sana. Sekta ya boda boda ni sekta ambayo imechangia pakubwa kuinua uchumi wa nchi yetu. Imechangia pakubwa pia kuimarisha uchumi wa jamii, na pia imetoa ajira kwa vijana ambao wamekuwa wakitangatanga mitaani bila ajira, na imeinua pia mapato ya jamii. Cha kusikitisha ni kwamba vijana hawa, wakiwa ni wasichana na wavulana ambao wanaendesha boda boda, ni watu ambao hata kupata leseni imekuwa ni shida. Kwa kusema kweli, maeneo mengi ambayo sisi wengine tumetoka, ni maeneo ambako barabara ni mbovu; ni maeneo ambako hata sisi tukiwa katika Bunge hii--- Ni mahali ambako inakubidi uache gari lako na kuchukua boda boda ndio uweze kuwafikia wananchi. Kwa hivyo, hizi boda boda haziwabebi tu wale watu wa chini. Wabunge watakubaliana nami haswa wale wa kutoka sehemu kavu, kwamba mara nyingi sisi tumelazimika kutumia boda boda ili kuwafikia wananchi wetu. Kwa hivyo, hizi boda boda zinapofanya ajali, hata sisi tukiwa Wabunge mara kwa mara tunapatikana katika hizo ajali. Cha kusitikisha ni kwamba hakuna mipango kabambe ya kutoa mafunzo na leseni kwa waendeshaji boda boda . Iwapo tunawataka hawa vijana wachangie uchumi wa nchi hii, ni lazima pia tuangalia maslahi yao. Ni lazima pia tuhakikishe kwamba wana usalama katika uendeshaji wa boda boda. Kwa hivyo, ombi langu ni kwamba Wabunge katika Bunge hili la Kitaifa la Kenya, na Serikali yetu, ambayo imechaguliwa na wananchi, waweke mipango kabambe kuhakikisha kwamba haswa utoaji leseni umepelekwa hadi vijijini. Kwa mfano, waendeshaji boda boda katika mji maarufu ambao nimetoka unaoitwa Doldol, inawabidi kwenda Nyeri ambayo iko katika Mkoa wa Kati kutafuta leseni. Labda ni kijana mmoja au wawili ambao watapata hizo leseni. Vijana wanapokosa hizi leseni, inakuwa ni kama kuwapatia polisi fursa ya kupata mapato yao ya kila siku kutoka kwa hawa vijana. Polisi wanapoishiwa na fedha mifukoni mwao, wanakumbuka kuna vijana ambao hawana leseni. Wanamwagika kwenya barabara na kuwadhulumu vijana wetu. Iwapo polisi atachukua Kshs500 au Kshs1,000 kutoka kwa mwendeshaji boda boda, siku hiyo, familia ya huyo mwendeshaji boda boda haitapata chakula chake cha kila siku. Ni ombi langu kwamba hili swala tuliitilie maanani, tulipitishe na tufuatilie kuona kwamba mafunzo kwa wendeshaji boda boda yametolewa. Pia, labda Serikali ilipe kitu kidogo ili gharama ya kupata leseni iwe ni ile ambayo hawa vijana wanaweza kuimudu na kupata leseni. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono mjadala huu."
}