GET /api/v0.1/hansard/entries/492198/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492198,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492198/?format=api",
    "text_counter": 134,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzunga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Kama walivyozungumza wenzangu, vijana wa boda boda wana mengi ambayo wanastahili kufanyiwa. Utapata Waheshimiwa mara nyingi ndio ambao wamesimamia yale matatizo ambayo yanawakumba hao vijana; kwamba mtu akiumia na ile pikipiki, Mheshimiwa ndiye anampeleka hospitali. Kama ni leseni, ni Mheshimiwa anashughulikia. Lakini kuna njia ambazo Serikali kupitia kwa hili Bunge inaweza kuboresha biashara hii iwe ya manufaa zaidi. Kwanza, utakuta kwa mfano kama kule kwetu Kaunti ya Kwale, hao vijana kupata leseni ni lazima waende Mombasa. Ingekuwa bora ikiwa kupitia kwa wizara inayohusika na usafiri, kungekuwa na shule maalum ya kuwapatia watoto hao mafunzo. Wakimaliza mafunzo yao, wapewe vifaa viwili au vitatu kama vile kofia ambayo ni lazima wawe nayo wakati wa kuendesha pikipiki. Pia abiria lazima awe nayo. Kwa nini ninapendekeza hivyo? Ukiangalia yule kijana wa boda boda kwanza, yeye hana ajira. Kwa hivyo, hana pesa za kununua vifaa vinavyohitajika. Wakipatiwa yale mafunzo na wakimaliza, wapatiwe zile kofia. Itakuwa pia tumewapunguzia ule mzigo ambao wako nao wa kuendesha pikipiki wakiwa na usalama wa miili yao na abiria wao. Lingine wizara hii inapaswa kushughulikia ni barabara zetu. Kusema kweli, barabara zetu zimechangia yale matatizo ambayo tuko nayo kutokana na uendeshaji wa pikipiki. Barabara zetu ni nyembamba na kwa hivyo, inamlazimu mwenye pikipiki aingiliane katikati na magari. Barabara zingine hasa kule mashinani ukiangalia vile zilitengenezwa, ni nyembamba na ni kama zina milima katikati. Kwa hivyo, yule mwenye pikipiki inamlazimu apitie katikati ya barabara na kama kuna magari pande zote za barabara, kuzihepa inakuwa ni shida na mwishowe pikipiki inapinduka na kuleta hatari ya mtu kuumia ama kufariki. Kwenye hospitali nyingi kuna vyumba vya malazi vinavyoitwa “ Boda Boda Ward”. Hiyo ni kwa sababu watu wote wanaolazwa kwenye vyumba hivyo wanaathirika kwenye ajali za pikipiki."
}