GET /api/v0.1/hansard/entries/492200/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 492200,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492200/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzunga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Kama walivyosema wenzangu, inafaa tuwe na hazina itakayotengwa na Bunge hili ili vijana waweze kuwa na pesa zao. Pesa zilizotengewa vijana kupitia Uwezo Fund ni ndogo mno na hazitawafikia watu wote. Kukiwa na fedha maalumu zitakazoelekezwa upande wa matatu na pikipiki, hazitaweza kuchukuliwa na watu wengine isipokuwa washikadau kwenye sekta hizo. Watapewa mikopo nafuu itakayowawezesha kufaidika na kujisimamia. Wataweza kununua vipuri vyao ama kuwa na maduka ambayo yatakuwa yakiuza vipuri vyao badala ya kufanya safari ndefu. Kwa mfano, kule kwetu Kwale, kununua vipuri ni lazima mwenye pikipiki atoke aende Mombasa kutafuta vipuri vya pikipiki. Pia watakuwa wanaweza kujifundisha mambo ya biashara na kuzipanua zile biashara zao. Naunga mkono mjadala huu na ni mjadala ambao una manufaa kwa vijana wetu na pia ukipanuliwa zaidi kulingana na mipangilio ambayo ipo ya Serikali, utaweza The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}