GET /api/v0.1/hansard/entries/492560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 492560,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492560/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Ahsante kwa kuniruhusu nichangie Hotuba ya Rais wetu, mhe Uhuru Kenyatta. Ningependa kumpongeza kwanza kwa sababu ametuonyesha mfano ambao tunastahili kufuata kama viongozi, kwamba sheria iko juu yetu sisi. Yeye alipojitoa mhanga kwenda Hague alikuwa anatuongoza kwa mfano bora. Ninampongeza kwa kitendo hicho. Rais alipomkabadhi msaidizi wake, mhe Ruto, mamlaka alikuwa anatuonyesha kwamba hana tamaa. Alituonyesha kwamba si lazima abaki kama Rais. Alituonyesha kwamba yuko tayari wakati wowote kutoa nafasi ili mtu mwingine ashike mamlaka. Hii ina maana kwamba hata baada ya wakati wake kuisha hatatuletea matatizo ya kulazimisha kubaki kwenye mamlaka; ataondoka kwenye kiti ili yule ambaye Wakenya watamchagua achukue nafasi. Jingine la kushangaza ni tabia aliyotuonyesha Rais Uhuru Kenyatta. Aliteremsha hadhi yake akawa sawa na mwananchi wa kijijini. Sisi tulioandamana naye kwenda Hague tulijionea kwa macho yetu kwa sababu tuliishi naye katika hoteli duni, tukala mtaani, na tukatembea kwa miguu. Hiyo ni heshima kubwa sana kwa sababu aliheshimu Umoja wa Afrika na kuonyesha kwamba asingepeleka Kenya kortini, ndiposa akaenda kama mtu binafsi. Ninampongeza kwa kitendo hicho. Lingine linalojitokeza, hasa kwa wale wanaosema kwamba Rais alihatarisha maisha yake ama wasimamazi wake walihatarisha maisha yake, ni kwamba Rais Uhuru anatawala watu anaowaamini. Yeye anaamini hawawezi kumdhuru, ndiposa alipowasili kutoka Hague aliingia kwenye gari lake na kupungia wananchi mkono wake. Yeye si Rais wa kimabavu. Hayaanzi sasa haya anayofanya Rais Uhuru. Alituonyesha alipokuja Pwani kwa maana tulienda naye hadi Public Beach kuogelea naye. Hii ina maana kwamba yeye ni Rais ambaye amejitolea ili amsikize mwananchi wa chini. Ukiongoza nchi kwa namna hiyo, basi utaelewa wanachotaka wananchi. Katika Hotuba yake amezungumzia pia kuhusu wale walioathirika, kwa mfano wale ambao wako kwenye kambi. Kesi haionyeshi kwamba ni ya maana kwa sababu tuliyasikia kwa masikio yetu na tukajionea. La muhimu ni Wakenya wawekwe mahali pamoja ili tuzungumziane na tuelewane ili yule ambaye aliumia apatiwe ridhaa yake kisha tuishi kama tulivyokuwa tukiishi zamani. Hizi kesi zikiendelea tutakuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}