GET /api/v0.1/hansard/entries/492581/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 492581,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492581/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Aburi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2901,
"legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
"slug": "lawrence-mpuru-aburi"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa muda, yangu nikushukuru Rais kwa ile kazi amefanyia Wakenya. Ya pili ni kile kitendo ambacho alifanya kabla hajaenda ng’ambo, kumwaachia Mhe. Samoei Ruto Serikali. Si wengi wanaweza kufanya hivyo. Hata wewe ukiwa mhe. huwezi kuwacha kiti chako na kwenda ng’ambo. Hiyo ni kuonyesha kwamba yeye ni mtu wa watu; hana mtoto wa mgongo wala wa tumbo; hana mtoto aliye na kamasi wala mate. Watoto wote wa Kenya ni wake. Jambo la tatu, aliingia gari bila walinda usalama na kupitia ule mlango ambao tunapitia tukienda ng’ambo. La nne, alirudi Kenya bila walinda usalama wowote mpaka akaingia Ikulu. Hii ni kuonyesha kwamba vita vya 2008 havikuwa vya Uhuru Kenyatta, William Ruto ama Raila; vilikuwa ni vita vya PNU na ODM. Alionyesha kwamba mkubwa wa Electoral Commission of Kenya (ECK) alitangaza ODM ilikuwa imeshinda uchaguzi na wakaanza kuimba wimbo, lakini baadaye akatangaza kuwa PNU walikuwa wameshinda, nao wakaanza kuimba wimbo; baadaye walikutana na wakaanza kupigana. Walipoanza kupigana, Uhuru Kenyatta hakuweko, William Ruto hakuweko na wengine pia hawakuweko; baadaye hatukusikia kuwa kile kikundi chote kingepelekwa The Hague. Wale walipelekwa Hague ni William Ruto na Uhuru Kenyatta. Hii Ndio sababu tunasema kama Wakenya tumekataa kutawaliwa vibya na wakoloni Waafrika wenye ngozi nyeusi. Wakati umefika sisi Wakenya tuweke ukenya wetu chini na tuseme sisi ni binadamu, na tushirikiane na watu wetu. Watu wanaona Uhuru Kenyatta akiitwa kule The Hague, na wengine wanapiga makofi na kusema kwamba anaenda kufungwa ili wachukue Serikali. Serikali haichukuliwi ovyo ovyo. Serikali huchungwa. Serikali ni kama mtoto mdogo. Uliona kitendo ambacho alifanya kilishtua Kenya yote. Kuna wengine wangeachiwa mamlaka vile Ruto aliachiwa wangesema eti Uhuru asikanyage uwanja wa ndege; Serikali yake The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}