GET /api/v0.1/hansard/entries/492582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 492582,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492582/?format=api",
"text_counter": 244,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Aburi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2901,
"legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
"slug": "lawrence-mpuru-aburi"
},
"content": "ingepinduliwa. Lakini hiki ni kitendo cha maana na nikiwa katika CORD naunga Serikali mkono. Kwa nini? Kwa sababu wameweza kuinua Wakenya na kutoa vitu vyote mezani. Kuna wengine wangechukua Serikali na kazi yao ingekuwa ni kufanya mambo chini ya meza. Lakini kwa sasa Jubilee inafanya mipango yake juu ya meza. Kwa njia gani? Angalia mambo ya pesa za kaunti. Kwa sasa Meru County ina Kshs5 billion; Kisumu ambao hawakumpigia kura, wana Kshs6 billion; Ukambani hawakumpigia kura na wana Kshs7 billion; Mombasa hawakumpigia kura na wana Kshs4 billion na yote ni Uhuru Kenyatta na William Ruto wameweka mezani. Lakini utasikia watu wakisema kwamba hakuna kitu Jubilee imefanya. Hakuna kwa nini? Eti kwa sababu wakati nyumba inajengwa, wakati msingi unachimbwa watu wengi hua hawajui kama ile nyumba itainuka. Wakati nyumba inaanza kuwekwa mawe na chuma na kuanza kuinuka, ndipo watu wanakubali kuwa kuna nyumba inayojengwa. Jubilee ilikuwa ikijenga nyumba; Ilikuwa ikichimba msingi. Sasa nyumba imeanza kuinuka na kuonyesha kwamba Uhuru Kenyatta anaweza kupeana Serikali. Anaweza kwenda bila walinda usalama. Hii ndio maana namwambia mheshimiwa asiseme Nyanza hawajafanyiwa kitu. Juzi wamepelekewa kshs7.6 billion na badala yao kupokea Rais kwa mikono miwili kama mtoto mdogo kwa sababu amewaletea pesa, walimpokea kwa viatu. Ndio maana ninasema hata wasingepewa hizo pesa. Zingekuja upande wa Meru ambako tuna taabu. Tuna taabu ya barabara, chakula na biashara ya miraa imefungwa kule ng’ambo. Tuna taabu ya vitu vingi. Kwa hivyo, nina imani na Rais wetu mpendwa, ambaye anatawala nchi hii na ninawaambia kwamba hakuna maana ya kubembeleza kile kikundi. Hakuna haja ya kumbembeleza punda kwa mteremko, mwachilie ateremke ukambembelezee kule chini."
}