GET /api/v0.1/hansard/entries/492583/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492583,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492583/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Kiptui",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 499,
        "legal_name": "Grace Jemutai Kiptui",
        "slug": "grace-jemutai-kiptui"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa hii nafasi. Ningetaka kuunga mkono hii Hotuba ya Rais, ambayo ilikuwa ni ya kusisimua na imejaa mawaidha. Kwanza, nilimwangalia Rais; nilikuwa nimeketi hapa na yeye pale. Nilipata wazo kwamba yeye ni kama Yesu, ambaye alikuwa ni mtoto wa Mungu, lakini akajishusha hadhi na kuwa mwanadamu. Tulikuwa na Rais ambaye alichukuwa kiapo kuongoza hii nchi lakini mwisho wa Hotuba yake akasema anampa msaidizi wake, Mhe. William Ruto, uongozi. Hilo lilikuwa tendo ambalo lilitufanya, kama Wakenya, kufikiria mara mbili na kuona kwamba Rais ambaye anatuongoza wakati huu ni mtu tofauti sana. Aliporudi juzi, alinena kwamba haijalishi ni nani anakalia kiti. Kilicho cha maana ni nani aliyekalia kiti hicho na anafanya nini. Hayo ni maneno niliojifunza. Najua kuna wenzangu ambao wako Bunge leo ama wametoka, lakini walisikia jambo la maana."
}