GET /api/v0.1/hansard/entries/492609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 492609,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492609/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "ni Kiswahili. Kipengele cha Pili kinasema kuwa lugha rasmi ni Kiswahili. Kumbukumbu ya Hotuba ya Rais iko tu kwa lugha ya Kimombo na Wakenya wengi hawatapata kubaini Rais alisema nini siku hiyo. Wacha nirejere mada yangu. Nauliza: “Je, ICC ina uwezo wa kuchambua, kuchunguza na kuishtaki kesi hii? Je, ICC ina ushahidi? Je, ICC imewahi kumfunga Rais ambaye si Mwafrika?” Hayo ni maswala ambayo yanaleta changamoto kubwa sana. Kwa wao wenyewe, tumesikia mambo mawili. Moja, Ocampo akasema kuwa alishurutishwa kufanya aliyoyafanya. Bi Bensouda kwa mkono wa kushoto, anasema kuwa hana ushahidi. Hata kwetu Kibera katika ile korti ya chini kabisa, iwapo mshitaki hana ushahidi, kesi ile inatupwa. Ningemuomba Bensouda asione haya, asimame kidete na atupe kesi hii. Haitampeleka mahali. Mzungumuzaji mmoja aliyenitangulia amesema kuwa Kifungu cha Pili Kipengele cha Sita kinasema kuwa Kenya imeratibu Mkataba wa Roma. Ni kweli Kenya imeratibu Mkataba wa Roma kama sheria lakini si kama Katiba. Katiba ya nchi, Kifungu cha 143(1), hairuhusu Rais wa Taifa anayehudumu kushtakiwa katika korti yoyote. Mkataba wa Roma na Korti ya Hague ni sheria na si Katiba. Waliosema hapa Kifungu cha Pili, wasome sheria vizuri. Hiyo itakuwa sheria chini ya Katiba ya Kenya. Ni nini chanzo cha taharuki na hamasa iliyowakumba Wakenya? Iwapo mahakama haina ushahidi na inataka kumbeba Rais wa Taifa kwenda kukaa ndani ya korti, hiyo ni hamasa na taharuki. Iwapo Rais wa Taifa atakwenda kukaa ndani ya korti, uhuru wetu utakuwa namna gani? Je, haki ya Wakenya milioni 40 waliomchagua kama Rais wao, watajisikia namna gani? Kwangu, Uhuru Kenyatta alikuwa Rais wangu lakini leo ni shujaa wangu. Amehifadhi hadhi na heshima ya Wakenya milioni 40. Hakuenda kupigiwa parapanda ndani ya korti ya wazungu. Jitihada aliyoifanya Uhuru ya amani Kenya, hatukuletewa na Hague. Wakenya wenyewe walisimama, wakashikana mikono na wakasema kuwa kuuana si suluhisho, tuje pamoja tugawane kikombe cha chai. Nimeambiwa hapa kuwa ni mchezo wa kuigiza kumuachia Ruto kiti cha Rais. Nataka wale ambao walisema hivyo wasome Kipengele 147(3) cha Katiba. Hii ni sheria ya Kenya wala si drama. Je, Ruto anastahili? Amesimama kidete akabeba Kenya. Hata Uhuru angebaki mwezi mzima huko, Kenya ingekuwa salama kwa sababu ni mtu anayestahili na anatosha. Mara hii, Kenya imepata mashujaa. Uchumi umeboreka Kenya na sasa Kenya ni miongoni mwa nchi kumi barani Afrika zenye uchumi bora. Hili halitambuliki leo kwa sababu vibaraka hawana masikio ya kusikia ukweli wala macho ya kuona haki. Wako hapa kupeleka parapanda kwa wazungu. Pelekeni lakini kesi hii itaanguka!"
}