GET /api/v0.1/hansard/entries/492770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492770,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492770/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Mhe. Spika, naungana na wenzangu pia kuhusu Harambee. Kwa kweli, Harambee zinasaidia Wakenya ambao hawajiwezi. Hii ni kwa sababu sisi kina mama wa kaunti tunatumia mifuko yetu. Hatuna ndururu katika CDF ama pesa za kaunti; kwa hivyo, Harambee ziendelee ndipo kile kidogo tulicho nacho kisaidie wale ambao hawajiwezi. Tuna watoto mayatima; tuna watoto hawajiwezi; tuna watoto wanafukuzwa shuleni. Kwa hivyo, nimeungana na wenzangu kusema ni muhimu tuendelee na Harambee. Kwa kweli pesa ambazo zinatoka CDF kama bursary na za kaunti hazitoshi. Hospitali zina wagonjwa na hawana pa kuelekea na ni lazima wawe na Harambee. Tukifunga Harambee, hao wagonjwa watasaidikaje? Watoto ambao hawajiwezi wataenda wapi? Kama kuna njia ya kuwa na sheria ya kuwasaidia wasiojiweza Harambeee iondolewe. Ninasema Harambee itaendelea. Kama kuna sheria nyingine, wale wasiojiweza pia watafutiwe njia ya kujisaidia. Kuna mambo mengi. Kuna mwenzangu ambaye ameongea kuhusu “Pesa Mashinani” na sahihi za watu; haiwezekani kuhusisha Harambee na hizi sahihi. Hakuna haja ya kuongea kuhusu jambo lililopita kitambo na kulihusisha na Harambee."
}