GET /api/v0.1/hansard/entries/492772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 492772,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492772/?format=api",
"text_counter": 79,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Spika, naomba nitoe mchango wangu kuhusu Hoja hii. Kitu cha kwanza, hata huenda ikawa wengi wa Wabunge ambao wako hapa, walisoma kupitia michango ya harambee. Ninajua kwamba ndugu yangu, Chris Wamalwa, alisomeshwa kwa Harambee. Hata ndani ya hili Bunge leo, tuna wageni ambao ni wanafunzi. Nimewaona huko juu kwa gallery ; wengi wao wanasomeshwa na fedha za Harambee. Wabunge wamejitoa muhanga ili kusomesha ndugu zao, watoto wa dada zao ama kaka zao. Kwa hivyo, kusema kuwa kuweko kwa Harambee kunaua ule moyo wa kutoa wa wananchi wetu si sawa; ninakubaliana na msemaji wa hapo awali. Alisema hata juu ya kichwa chako kuna neno “Harambee”. Sisi ni nani tuanze kusema hatutaki Harambee? Ningeomba niisome hiyo barua kwa kina na niielewe. Inasema tusitoe Harambee ama tusiombe pesa za kutoa katika Harambee? Vile nimeielewa, anaomba tusiende kutafuta hela huko nje za kutoa kwenye michango; lakini kama mimi binafsi nina hela The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}