GET /api/v0.1/hansard/entries/492773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492773,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492773/?format=api",
    "text_counter": 80,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "zangu, nina nia ya kumsaidia mtu fulani, nani hapa nchini anaweza kunizuia kumsaidia mtu fulani? Hata Jumapili ijayo, Rais atakuwa katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni, na atakuwa anachangisha pesa. Mnataka kuniambia nisiende nikachangie shule? Mimi naye tutapelekwa kortini? Kama vile mwenzangu amesema, ni kweli kuwa hiyo barua ina ubaguzi. Imelenga Wabunge peke yao; imeacha watu wengine. Naomba tuangalie hilo jambo vizuri; ikiwa Wabunge wamejitolea kutoa mchango wao kusaidia wagonjwa, shule na kadhalika wasiwekewe vikwazo na mtu yeyote. Naomba ndugu yetu wakati huu aanze kufikiria mwenzake. Alianza kuzozana na Wabunge katika Bunge la Kumi na kilichompata kilikuwa ni kuondolewa kutoka kazi yake. Singependa twende njia hiyo; inafaa tuwe na tahadhari."
}