GET /api/v0.1/hansard/entries/492962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492962,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492962/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Kama Katibu wa Wizara, Mhesimiwa Charity Ngilu amekuja hapa akajieleza na wenzake wawili walionekana hapa basi kilichowafanya watoweke ni nini? Ni uoga ama nikutuheshimu Bunge ama nini kimetokea? Ndio maana nilikuwa naomba Kiranja wa Walio Wengi Bungeni na Walio Wachache--- Naomba nifafanue, sisi mrengo wetu mnatuita wachache hapa Bungeni lakini uko nje ndio tulio wengi. Kwa hivyo, Kiranja wa Walio Wengi ndani ya Bunge ningeomba afafanulie Bunge ni nini kimewafanya hawa wenzetu Makatibu wakaondoka bila kuja kufafanulia Bunge yale ambayo walikuwa wameitiwa. Hata kama walikuwa wanaondoka wangeomba radhi. Wangeeleza, “mna mambo yametokea dharura na inatubidi tuondoke na tunaomba msamaha ili tuje wakati mwingine tujieleze yale ambayo yametuvika”. Wamepotea hivi hivi. Je, ni watu wenye nidhamu ama ni watu tuu wanachukulia Bunge kama ni kitu, ama ni watu wanakutana tuu kupoteze muda?"
}