GET /api/v0.1/hansard/entries/492963/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492963,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492963/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ni ombi langu kuwa hawa waje tena wajieleze na wachukuliwe sheria za kinidhamu. Mwenzangu Mheshimiwa Nyokabi alisema kuwa Serikali hii ya Jubilee iko katika nguzo za uwajibikaji na uwazi. Nashukuru na ni vizuri. Kama iko katika nguzo za uwajibikaji na uwazi mbona watu wao hivi leo asubuhi wakaogopa kuja mbele ya kamati ya Bunge? Walikuwa wamepata wakati unaofaa waje wajieleze na waonyeshe kuwa Serikali ya Jubilee imefanya hili na inataka kutekeleza haya na hatufichi chochote lakini huu uoga umetokea wapi? Ni nini wanachoficha?"
}