GET /api/v0.1/hansard/entries/492968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 492968,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/492968/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, tulikuwa na kikao hapa Jumatatu iliyopita ambacho kiliandaliwa na Mheshimiwa Spika. Makatibu wa Wizara wakaja wote na wakaelezwa kwa nini tumebadilisha sheria zetu za Bunge. Wanakuja kwa kamati andalizi ya Wabunge wote ili wajieleze. Wakafafanuliwa kila kitu. Jana na leo katika magazeti tunasoma kuwa mmoja wa Makatibu ambaye ni kinara wa Jubilee anawaomba hawa Makatibu wa Wizara wasije Bungeni. Yeye mwenyewe kwa nini awaelekeze? Kwa hivyo, kuna utata mkubwa ambao tungeomba Bunge iutatue. Inafaa wafahamu kuwa wakija hapa ni kujibu maswala ambayo Wabunge wangependa yafafanuliwe. Kwa haya mengi Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, naomba kuweka tamati."
}