GET /api/v0.1/hansard/entries/493243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 493243,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493243/?format=api",
    "text_counter": 240,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mositet",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 608,
        "legal_name": "Peter Korinko Mositet",
        "slug": "peter-korinko-mositet"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii nichangie Hotuba ya Rais katika kikao cha pamoja cha Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Rais alifanya jambo la busara na alifuata Katiba inavyosema kwamba ikifika wakati ambapo taifa linahitaji kusikia kutoka kwake, anaweza kupitia Bunge. Bw. Naibu Spika, Rais wetu alifanya hivyo wakati ambapo nchi nzima ilikuwa imeingiwa na baridi na hofu. Kila mtu nchini alikuwa anaangalia upande upande – wale walio katika upinzani na wale walio katika mrengo wa Jubilee – wote tulikuwa tumeshikwa hofu tukiulizana je, ICC inatutakia nini? Je, inataka Rais wetu aende ICC ilhali tumemchagua kama Rais? Kwa sababu hiyo, Rais alifanya jambo la busara sana kwa kuitisha kikao cha pamoja cha Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa ili azungumzie yale aliyoweza kusema. Maneno yake yaliweza kuchangia na kutupatia mwelekeo kama taifa. Maneno yake yaliweza kuunganisha taifa na tukaelewa kwamba hata kama ICC iko, taifa la Kenya litasimama wakati wowote. Bw. Naibu Spika, Rais alisema kwamba mambo ya ICC ni mambo yake ya kibinafsi na hii ndio sababu aliyehitajika kufika mbele ya mahakama hiyo kama mtu binafsi na wala si uongozi wa nchi. Kuambatana na busara yake, alimteua Naibu Rais kuwa kaimu Rais. Alifanya vile sisi hatukufikiria. Hata nchi nzima haikufikiria angefanya hivyo. Tulifikiria kuwa Rais ataenda ICC akiwa Rais hata bila ya kusema kwamba atamwachia naibu wake usukani. Bw. Naibu Spika, kwa wale wanaosema kwamba Rais hakufanya vile; ati ilikuwa tu ni sarakasi, hiyo si kweli kwa sababu wakati alipomuachia Naibu wake ashikilia hatamu ya uongozi. Naibu Rasi hakuitwa Naibu Rais tena, bali aliitwa kaimu Rais. Kwa hivyo, ni vizuri sana tujue kwamba hakukuwa na sarakasi pale. Rais wetu mwenyewe alijishusha kabisa. Kitendo hicho kinatuonyesha kwamba Rasi wetu aliona kwamba ilifika wakati lazima hata Katiba yetu itekelezwe vile ambavyo hatukufikiria. Kuna wakati sisi husoma vipengele vya Katiba na hatujui vile vinaweza kutekelezwa."
}