GET /api/v0.1/hansard/entries/493248/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 493248,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493248/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa kufanya vile, alituonyesha kwamba kweli yeye ni mfuasi wa Katiba kabisa. Kuna wengine ambao waliwahimiza viongozi wasihudhurie. Ningependa kuwashukuru Wabunge wote wa upande wa CORD na Jubilee kwa sababu walionyesha ushujaa. Walionyesha uzalendo na wakajitokeza kumsikiza Rais. Waliona kwamba Rais anaipenda nchi hii, ana maono ya nchi hii na hajitakii makuu lakini kuna yale anayoitakia nchi hii. Naikumbuka siku ambayo Rais alisema atampa Naibu wake madaraka ili aiongoze nchi. Niliyaona machozi yakiwadondoka Wabunge wengi kwa maana hawangefikiria kuwa maneno hayo yangenenwa na mtu ambaye ni Rais. Aliyafanya hayo yote kwa kuwa yeye ni mzalendo. Huyu ni mtu ambaye anaipenda nchi yake. Huyu ni mtu ambaye anajua utafika wakati ambapo yeye hatakuwa Rais lakini angependa kuiona nchi imesimama imara. Alifikiria na kushangaa vile nchi ingeachwa akienda huko The Hague. Kiongozi wa Wachache alisema hakuona upanga ukipeanwa. Anafaa kujua kwamba kuna yale kaimu Rais anafaa kuyafanya na yale ambayo hafai kuyafanya. Rais pia ni Mkuu wa Majeshi. Kwa hivyo, bado alikuwa ameyashikilia mamlaka hayo. Kwa hivyo, upanga haungepeanwa. Tulishuhudia Naibu Rais akipewa madaraka ya kuiongoza nchi. Pia tuliona kwamba aliyepewa ni mtu mwenye hekima kabisa; mtu ambaye ni mpole. Huyu ni mtu ambaye anaipenda nchi yake kabisa. Tuliona viongozi ambao tunafaa kuwapigia kura. Ningependa kusema kwamba ICC ni jambo ambalo limekuwa likitusumbua. Tumekuwa tukijiuliza mambo ya ICC na kushangaa korti hiyo inataka kutoka nchi yetu. Ukiangalia mahali tumefika utaona kwamba kama mambo ya ICC yangeendelea na kama Rais hangeshikana mikono na Naibu wake katika maombi kuhakikisha kwamba jamii zimerudiana, na kuhakikisha kwamba mikoa ya Bonde la Ufa na ile ya kati zimeungana kabisa, tungekuwa wapi? Hakuna wakati ICC imesema kwamba kwa sababu kulitokea mambo yale, wananchi wanafaa kushikana na kuwa kitu kimoja. Nawashukuru Rais wetu na Naibu wake. Mungu aliwaonyesha kwamba ni jukumu lao kuliunganisha taifa hili. Maombi ya wale ambao wanamuogopa Mungu; mimi ni mmoja wao. Tuna Waislamu na Wakristu ambao wanaomba kabisa. Kusema kweli, tumeyaona mengi yakifanyika katika nchi hii. Haya yote yameunganisha taifa hili kabisa tukawa kitu kimoja. Tumeona ushindi mkubwa katika taifa hili. Nikiangalia, naona ICC ilikuwa ilete udhaifu mkubwa lakini kupitia maombi, hayo yote yameshindwa. Kupitia maombi, tumeona Rais na Naibu wake walichaguliwa na Wakenya wote waliona. Kwa hayo yote, namshukuru Mwenyezi Mungu. Ningependa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}