GET /api/v0.1/hansard/entries/493286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 493286,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493286/?format=api",
    "text_counter": 283,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "October 21, 2014 SENATE DEBATES 52 Sen. Njoroge",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja iliyoko mbele ya Seneti. Kwanza, napenda kuunga mkono Hotuba ya Rais iliyotolewa tarehe sita Oktoba. Rais alionyesha ujasiri mkuu na heshima yake kwa Bunge letu – lile la Kitaifa na pia Bunge la Seneti. Bw. Spika, ujasiri ulioonyeshwa na viongozi wetu, haswa Rais wetu, kwa kukubali kuelekea kule The Hague kuhudhuria kesi katika mahakama ya ICC ilikuwa jambo la busara sana. Lakini hata wakati ninapofikiria kuondoa siasa katika ile korti kuhusiana na mashtaka yanayomkabili Rais, pia ninashawishiwa na lile korti ama kiongozi wa mashtaka alipokuwa anaendelea kutoa ombi lake kwa majaji ili waweze kuahirisha ile kesi inayomhusu Rais. Bw. Naibu Spika, nakumbuka wakati mmoja ambapo kiongozi wa mashtaka aliwaeleza majaji wapeane muda kwa sababu mwaka wa 2017 unakuja na kutakuwa na uchaguzi hapa Kenya. Kwa hivyo, upande wa mashtaka ni kama ulikuwa unaahidi kwamba tukiingia katika uchaguzi wa mwaka 2017, Rais asipochaguliwa tena, pengine watapata ushahidi waliokuwa wakitarajia. Upande wa The Hague ulijaribu kushawisha majaji kwamba jambo hili linahusishwa na siasa. Licha ya hayo, niliona kwamba upande wa mashtaka umeahidiwa na watu fulani kwamba Rais akiondoka katika mamlaka, watapeana ushahidi katika The Hague. Walijaribu kuwasawisha majaji ili wakubali kuhahirisha kesi wakitarajia kwamba uchaguzi ukija katika mwaka wa 2017, kutakuwa na kiongozi tofauti na si Rais Uhuru Muigai Kenyatta. Bw. Spika wa Muda, viongozi wameonyesha ujasiri mwingi ambao ni wa hali ya juu. Pia, ningependa kuwaunga mkono. Kama vile tumesikia mali ya Seneta mmoja ya dhamana ya Kshs25 milioni iliharibiwa huko Migori. Ningependa kujiuliza kama mambo hayo yalifanywa na Rais na Naibu wake. Ni Rais na Naibu wake ambao walienda Migori kuharibu mali? Tumesikia kwamba huko Kisumu na kwingineko kama Mombasa kulikuwa na ghasia. Vile ninavyoona, jambo hili lilienda kisiasa. Nashangaa kwa sababu wale waliofanya kitendo hicho hawakushatakiwa. Wao walibaki wapi wengine walipokuwa wakishtakiwa? Mimi kama mkaaji wa Naivasha, sehemu moja ambayo Rais anatajwa kuhusika nilishangaa kwa sababu hakuna wakati Rais alikuja Naivasha. Ni jambo la kusikitisha wakati Rais anatajwa katika mambo ambayo hayawezi kuthibitishwa kortini. Licha ya hayo, ni jambo la kushangaza na kilio kilichokuwa katika upande wa mashtaka. Walikuwa wakitaka kujua kama mshtakiwa angewasaidia na ushahidi. Hilo ni jambo ambalo katika sheria halikubaliwi. Mtu hawezi kumshtaki mtu, bila ushahidi halafu kuanza kumtisha mshtakiwa kutoa ushahidi ili aweze kuendelea na mashtaka. Hilo ni jambo la kushangaza sana. Ninaamini pia viongozi wetu ni wacha Mungu. Hiyo ndio sababu wale ambao wamewashtaki hawana ushahidi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}