GET /api/v0.1/hansard/entries/493336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 493336,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493336/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ahsante, Mhe. Spika. Naomba nami nichukue nafasi hii kupeana rambirambi zangu kwa familia ya kaka yetu, ndugu yetu mpendwa, Prof. Ali Mazrui. Wengi wetu tulimfahamu Prof. Ali Mazrui tukiwa chuoni kama wanafunzi wakati alikuja kupeana mijadala kadha wa kadha, ijapokua wakati huo ilikua vigumu sana kwa mtu msomi mwenye fikira tofauti na za uongozi, kukubaliwa kuendelea kupeana mijadaala. Ilibidi mara nyingi Prof. Ali Mazrui awe nje ya nchi kwa kueneza na kufunza watu ambao walikua wanahitaji elimu yake na ufasaha wake. Tutakubali kuwa Prof. Ali Mazrui alikua amesifika. Alikua ana sifa za hali ya juu. Prof. Mazrui alikua ametukuzwa na watu kwa ule ufasaha wake na vile alivyo kuwa anawajibika katika shughuli zake za kila siku. Prof. Ali Mazrui alikua ametamba katika shughuli za elimu. Nani angeweza kutamba mbele ya Prof. Ali Mazrui kwa kisomo alichokua nacho? Baada ya kutamba kimasomo, alikua ameheshimika kwa sababu ya maadili yake. Ufisadi, kama wenzangu walivyotangulia kusema, ulikuwa si mmoja wa ngao zake katika maisha. Mara nyingi alikosana na wengi kwa sababu ya kuzungumza kwa undani kuhusu ufisadi. Aliwakemea wote ambao walikua wanajaribu kuendesha ufisadi. Tutakubaliana kuwa, kifo cha Prof. Ali Mazrui kimepokonya nchi hii na ulimwengu mzima na wasomi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}