GET /api/v0.1/hansard/entries/493337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 493337,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493337/?format=api",
"text_counter": 38,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "wote kwa ujumla, Mwanakenya shupavu; shujaa. Nina imani atawekwa katika kumbukumbu zetu nchini kuwa mmoja wa watu wa Kenya ambao wamejibidisha iwezekanavyo katika mrengo wa elimu. La mwisho, naomba wenzetu ambao pia nao wamesoma, wajaribu wawezavyo kuiga mfano wa Prof. Ali Mazrui. Si mtu ambaye alikuwa anataka kujilimbikiza mali ya ulimwengu. Sote tunajua tunaiacha, bali aliishi kama mtu mnyenyekevu, mpole mwenye hekima na busara, na mstaarabu. Yote haya ni maadili ambayo yalikua na Prof. Ali Mazrui. Kwa hayo machache, naomba kutoa pole zangu kwa familia na nchi nzima kwa ujumla. Ahsante Mhe. Spika."
}