GET /api/v0.1/hansard/entries/493903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 493903,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493903/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, mara nyingi, unapoenda kwenu kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Eldoret, hutumia ndege gani? Utaona kwamba ni shirika moja tu ambalo limepewa nafasi – Kenya Airways. Kampuni nyingine inayoruhusiwa kupeleka ndege huko ni Flight 540. Mimi na mhe. Mwinyi tukichukua mkopo kutoka kwa benki na kununua ndege hatuwezi kuruhusiwa kutumia anga ya nchi hii kwa sababu imetengewa Kenya Airways. Kwa hivyo, ninatoa changamoto kwa Serikali iweke anga yetu wazi kwa wale watu ambao wangependa kushiriki katika biashara ya usafiri wa ndege ili nauli za ndege zishuke."
}