GET /api/v0.1/hansard/entries/493956/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 493956,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493956/?format=api",
    "text_counter": 43,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Ninachukua nafasi hii kuunga mkono Hotuba iliyotelewa na Mhe. Rais wa Kenya. Kwanza ningependa kuwapongeza Wabunge wa mrengo wa CORD ambao walikuja kuhudhuria kikao hiko kufuatia mwito wa Rais kwa sababu yeye ni Rais wa kila mtu katika taifa hili. Ilikuwa na faida gani kutengewa viti kwenye Bunge na kuamua kutohudhuria na bado unaonekana kwenye runinga ukiongea mambo mengine. Ilikuwa ni aibu kubwa sana. Kwa nini msiitikie mwito badala ya kukaa nyumbani na kujifanya hamna haja huku mnataka kujua kile ambacho anahutubia Bunge. Hilo ni jambo la huzuni sana. Bw. Spika, Rais wa Kenya alijitoa mhanga na kuonyesha ushujaa wake. Tunajua kwamba si rahisi kiongozi kupeana nafasi kwa mwenzake akalie kiti chake cha uongozi. Mbona wewe hunikaribishi kwenye kiti cha Spika ili nikalie hata kwa dakika mbili ili katika historia ijulikane kwamba nimewahi kukalia kiti cha Spika. Ukiangalia historia ya nchi ya Kenya, kuna watu ambao wakati huu wameaga dunia, lakini wangepewa hicho kiti kwa dakika mbili tu, wangefufuka kutoka makaburini mwao. Hilo ni jambo la kihistoria ambalo Wakenya watalikumbuka milele. Dunia nzima itakumbuka ule uhusiano wa Rais na Naibu wa Rais kama ule ambao hauna kifani; ni undugu na ujamaa ambao hakuna mtu anayeweza kueleza. Bw. Spika wakati Kenya inashinda medali michezoni sisi sote hufurahia. Vile vile tukifiwa, sisi sote huwa na huzuni kwamba mmoja wetu amefariki. Sioni ni kwa nini wakati huu tuna dua ya kuku au dua mbaya wakati mmoja wetu anatarajia kuhukumiwa kule The Hague. Ni lazima tuwe wazalendo; jambo likimkabidhi mwenzetu inafaa sisi sote tusaidiane kama jamii moja. Pia ningependa kusema kwamba, inafaa tuwaangalie wale waathiriwa wa michafuko ya 2007/2008. Watu hao wakiweza kuishi vizuri kama Wakenya wenzao, tutafutika machozi kidogo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}