GET /api/v0.1/hansard/entries/493958/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 493958,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/493958/?format=api",
    "text_counter": 45,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, ninaomba Wakenya waendelee kuomba na kushikamana. Kama tunavyojua, umoja ni nguvu. Tukishikamana sote, tutafaulu kwa sababu hakuna mtu ambaye atatoka nje ya Kenya na aje kutujengea Kenya yetu isipokuwa sisi wenyewe. Ni lazima tuungane mkono na tuwapatie nguvu hawa viongozi wetu. Yule atakayechukua mamlaka 2017, pia tutamuunga mkono. Hakuna jambo nzuri kama kuwa katika Serikali. Ninawaomba wale ambao wanajiingiza kwenye hiyo kesi kwa sababu hao ni wa mrengo fulani waunge Serikali mkono ili tushughulikie maslahi ya Wakenya ili ile manifesto ya Jubilee itimie na tuishi kwa amani. Hii ni kwa sababu bila amani hatuwezi kupiga hatua yoyote. Bw. Spika, mifano imetolewa hapa na hakuna mtu ambaye anaweza kupeana kiti chake. Hakuna mtu ambaye angependa kutolewa nyama mdomoni. Lakini ukiona Rais amepeana kiti chake, huyo ni Rais ambaye lazima tumheshimu. Huyo ni Rais wa kipekee. Hata lile gari lako Bw. Spika, ama langu hatuwezi kumbalia mtu mwingine alikalie. Kwa hivyo, huyu ni kiongozi wa kimaajabu. Halafu pia naomba kumpa kongole makamu wetu wa Rais. Kile kiti kilikuwa kimempendeza kweli. Mimi sikujua kama angeenda kumpokea Rais wake. Hawa ni viongozi ambao lazima Wakenya waige mifano yao. Bw. Spikla, naomba kila mwananchi wa Kenya achukue mfano wa viongozi hao tulio nao. Ulikuwa ni mfano mkubwa na funzo kubwa kwa taifa hili. Hii ni dhihirisho kubwa kuwa tuna viongozi ambao ni wa kipekee. Kuna baadhi ya watu ambao dua zao ni kuona kuna uhasama kati ya Rais na Naibu wa Rais. Hawafurahii kuona uwelewano kati ya viongozi hawa wawili. Wengine wanadai kuna mgongano kati yao. Lakini kitendo hiki cha Rais kilidhihirisha wazi kuwa watu wanasema uongo. Ninatoa hongera yangu kubwa isiyo na kifani kwa kuwa hawa ni viongozi wanaofaa kuigwa na wengi. Tukiangalia mpaka mashinani kule kwa Kaunti, wakati mwingine unaona kuna kutoelewana kati ya viongozi wetu. Mtu mmoja akiwa juu, hamtaki yule mwingine atambulike. Kwa hivyo, hili ni funzo ambalo limekuja na limeonyesha kwamba Rais wetu anaichukulia nchi nambari moja kuliko nafsi yake."
}