GET /api/v0.1/hansard/entries/494661/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 494661,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/494661/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wangari",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13123,
        "legal_name": "Martha Wangari",
        "slug": "martha-wangari"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika. Ningependa kumshukuru Sen. Wetangula kwa kuleta Hoja hii mbele yetu. Kwa wale ambao hawakuweko katika miaka ya 1960s, kile tumefanya ni kusoma mambo yanayomhusu. Ningependa kuungana na wenzangu kwa kutuma rambi rambi. Ali Mazrui alikuwa na talanta ambayo sio wengi waliyo nayo. Alikuwa msomi, mtaalamu na sio wa Kenya tu, bali wa Afrika na dunia nzima. Nimesoma vitabu vyake na hakuandika tu kuhusu Afrika; ameandika vitabu vya dini ya Kiislamu hata kiyahudi. Ninadhani itakuwa muda kabla tuwe na mtu kama huyu. Ameandika vitabu zaidi ya 20 na makala mengi ambayo nimeyasoma na kusikiza. Sisi kama nchi tunafaa kujifunza sana haswa Serikali ambavyo ilivyo sasa. Serikali hii imefanya muhula wake wa kwanza. Hatujafanya vizuri kuwatambua mashujaa ambao wameweka nchi hii mahali ilipo. Ninadhani mambo ya Ali Mazrui yatatufungua macho, wale ambao tuko uongozini leo na wale ambao watatufuata kesho ili watambue mashujaa wa nchi. Kila mwaka tutasherehekea siku ya Mashujaa ambayo tulikuwa tukiita Kenyatta"
}