GET /api/v0.1/hansard/entries/494663/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 494663,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/494663/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wangari",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13123,
"legal_name": "Martha Wangari",
"slug": "martha-wangari"
},
"content": ". Ni wangapi tumewatambua ambao walifanya kazi kwa kalamu na kutaja mambo ambayo hayangesikizwa? Watu hawa walikuwa na ujasiri wa kuyasema. Wakati alipopewa kazi ya kuwa Chancellor wa Chuo Kikuu cha Kenyatta, alikuwa na haki ya kuikataa kazi hiyo akikumbuka vile alivyoumizwa hapo mbeleni. Lakini kwa sababu alikuwa na mapenzi kwa nchi yake na kwa vile yeye ni mzalendo, aliichukuwa kazi hiyo na kujifanya mdogo hadi akakiongoza chuo cha Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT). Niliyafuata mazishi yake kwenye television kwa sababu singeweza kuhudhuria. Niliwasikiza wale ambao walikuwa wakimjua kibinafsi na nikatamani watu kuongea mazuri kunihusu wakati nitakapokuwa nikiwekwa kwa kaburi. Sisi wote tumepewa changamoto. Lazima tuhakikishe kwamba hata tukifa, hatufi na mambo ambayo tumeona duniani. Tunaweza kuyaandika ili yasomwe na watoto wetu. Mambo ya Ali Mazrui yatasomwa na watoto wetu na vizazi vingine vijavyo. Ningependa kusema kwamba Mungu amlaze mahali pema. Ningependa kutuma rambi rambi zangu kwa familia yake na kwa wale ambao walimtambua alipokuwa hai. Asante, Bw. Spika."
}