GET /api/v0.1/hansard/entries/494669/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 494669,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/494669/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "vifo vya ajabu. Sisi twamsifu Mungu kwa maisha ya msomi huyu wa Kenya aliyezaliwa, kukuzwa na kupata nafasi ya kuishi miaka 80. Kuishi miaka 80 ni bahati. Kwa hivyo, badala ya kulia sana na kububujikwa na machozi, tunafaa kusherehekea maisha ya mkombozi huyu wa akili za binadamu. Mawazo yake huenda yasitambuliwe na kueleweka kwa vizazi kwa sababu akili zake zilikuwa za mbali. Marehemu Einstein, yule mwanafisia mkuu hakueleweka. Alipokufa, walitoa bongo zake wakaweka nje kusudi wajaribu kuona ni nini kilichomfanya kuwa hivyo. Huenda isiwe mila na desturi ya Mwafrika, tungemfanyia mzalendo huyu hivyo kusudi tutambue hasa ni nini kilichomfanya kuwa na hekima na uerevu kiasi hicho. Lakini maisha yake bado yataangaza kwa vitabu na makaratasi aliyoandika ili yasomwe na vizazi na sio tu wanakenya, bali ulimwengu mzima. Yeye hakufa hivyo. Ameacha mwanga na akili nyingi kwa vitabu zaidi 30 alivyoviandika. Mimi sikuwa na bahati ya kuwa mwanafunzi wa msomi huyu kwa sababu ya kazi niliyoisomea. Lakini fikira na uzalendo wake ulidhihirika na kusikika ulimwengu mzima mpaka viongozi wetu hawangemuelewa. Walimwita katili ambaye hakutakikana. Basi ilibidi atoke na kuenda katika nchi ambazo zingempa nafasi ya kujieleza. Hiyo ni aibu kubwa. Ninashukuru vile Sen. Wetangula ameyanakili maisha yake. Ametoa usia Kimazrui ingawa alimwita mdogo wake. Huyu ndiye Mazrui kwa sababu ameangaza maisha yake kwa muda mfupi na kuyaeleza vile tunavyoelewa wale ambao hatukukutana naye uso kwa uso, msomi huyu mkuu wa Afrika na ulimwengu mzima. Yetu ni kumkumbu na pengine kutoa rambi rambi zetu kwa jamii na marafiki ambao walimpoteza msomi huyu. Tunawaombea baraka za Mungu. Wasilie sana. Ninashukuru."
}