GET /api/v0.1/hansard/entries/494723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 494723,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/494723/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi kuunga Hoja hii mkono ambayo imeletwa na Sen. Wetangula. Kabla sijatoa risala zangu za rambi rambi, ningependa kumpongeza Sen. Wetangula kwa kufikiria kuleta Hoja hii ili tuzungumze kama viongozi na Maseneta wa nchi hii. Ningependa kutoa risala zangu za rambi rambi kwa jamii na marafiki na watu wa Kaunti ya Mombasa kwa kupoteza mtu ambaye alikuwa msomi na mtafiti. Mimi najua kwamba utafiti wake na usomi wake umewajenga wananchi wa nchi hii. Yeye alituonyesha uzalendo hata ingawa alipitia shida nyingi. Ingawa aliishi katika nchi ya nje, alionyesha uzalendo mwingi. Kama Seneti na viongozi wa nchi hii, yeye anafaa kutambuliwa. Ningependa kusema pia haya tu hayatoshi. Wakati mwingine, tunafaa kuwatambua wale ambao wanaifanyia nchi hii kazi. Kuna wale ambao wameeneza mambo ya amani katika nchi yetu na mambo mengine ambayo yametusaidia katika nchi ya Kenya. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Seneta ambaye ameleta Hoja hii. Ningependa kuwashukuru wote ambao wameongea kuhusu Hoja hii. Ninatoa rambi rambi kwa niaba ya Kaunti ya Nakuru."
}