GET /api/v0.1/hansard/entries/494818/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 494818,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/494818/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Kusini ambaye bado ni mgeni, hajaelewa sana kanuni zinavyosema na kwa hivyo ni vizuri Wabunge wenzangu wamuelewe. Sisi sote tunaumwa na roho kuwa maafisa hawa hawajaenda bado kwenye mafunzo hayo lakini vile vile, ni muhimu tukumbuke kwamba ni lazima tugawanyane majukumu, mahakama wafanye kazi yao na sisi Wabunge pia tufanye kazi yetu. Kitu ningeomba ni mahakama iharakishe ili wale waliochaguliwa kwenda kwenye mafunzo waweze kwenda haraka iwezekanavyo. Vile vile, Mhe. Spika, wewe kama Spika wetu umekuwa ukiheshimu kanuni za Bunge na sheria za nchi hii kwa hivyo hakuna sababu ya mtu yeyote kusimama, kukulenga na kukurushia maneno ambayo si ya haki na ambayo ni bughudha. Mhe. Spika, ninaomba wenzangu tutulie, tumuelewe mwenzetu na tutulize zile duku duku tulizo nazo kuhusu maafisa hawa. Asante sana."
}