GET /api/v0.1/hansard/entries/494982/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 494982,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/494982/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii kuhusu maji. Kama wenzangu walivyosema, maji ni uhai. Sijui ni sheria gani ambayo itatumiwa ili Wakenya wote wapate maji. Shida ya maji iko kila mahali. Ukipita popote katika Kenya, kuna shida ya maji. Shida hii ni kubwa katika jamii ya wafugaji. Mtu ambaye ameteseka katika Kenya hii ni mama mfugaji. Mpaka wakati huu, utakuta watu wanatembea kwa siku tatu kutafuta maji. Akina mama wanazunguka na punda wakitafuta maji. Hata hivyo, ni vigumu sana kutoa maji kwa shimo na watu wanne ndio wanaweza kutoa maji kutoka ndani ya shimo. Kaunti haziwezi kusaidia katika mambo ya maji. Mambo ya maji yanafaa yabaki katika Serikali kuu. Maji ni muhimu kwa maisha ya binadamu. Kwa mfano, hospitali haziwezi kuwahudumia watu bila maji. Usafi wowote unahitaji maji kama vile vyoo, watoto kwenda shule na pia watoto kuzaliwa. Tunafaa kutafuta njia ya kuwawezesha Wakenya kupata maji. Jambo lingine ambalo linatushangaza ni kuwa mvua ikinyesha, kunaambiwa kuwa maji yamebeba nyumba na ng’ombe. Ni muhimu tutafute njia ya kuzuia maji mvua ikinyesha. Ardhi imeharibiwa na binadamu. Watu wamekata miti na ili kupanda miti mingine ni lazima tuwe na maji. Mvua ikinyesha, hakuna kizuizi cha kuzuia maji. Maji hayo huaenda mpaka baharini. Mvua ikikosekana, ukame unaingia na kizuizi cha kuzuia maji. Vizuizi ndivyo zinafaa kusaidia Wakenya. Wakati wa ukoloni, katika kaunti ya Samburu, tulikuwa na vizuizi vya kuzuia maji karibu 94. Sasa hivi, ni vitano tu ambayo vinaweza kuwa na maji. Vingine vyote vimefunga. Vizuizi vya kuzuilia maji ni muhimu sana. Kule kwetu, visima vya maji vinachimbwa lakini hakuna maji. Wakati mwingine maji yakipatikana, yana chumvi nyingi na watu hawawezi kuyanywa. Sehemu nyingine, watu hawakunywi maji ya kisima kwa sababu yamejaa chumvi. Kwa hivyo, cha muhimu ni kuwa na mabwawa mengi ya kuzuilia maji, haswa katika jamii ya wafugaji. Sisi tuna ardhi. Ardhi ya wafugaji haijalishi. Tuna ardhi ya kuchimba mabwawa. Mwenzangu amesema kuwa ng’ombe wanatembea mpaka Nairobi. Huu ni ukweli. Juzi, watu wangu wameniambia niende nikawaombee nyasi kwa kambi ya GSU. Wakati wanapata nyasi, hawana maji. Kwa hivyo, maji ni muhimu sana katika Kenya yetu. Inafaa tujue ni njia gani ambayo tutatumia ili kila mtu apate maji. Akina mama wa kwangu, wameumia sana. Kule kwetu, mwanaume hawezi kwenda kutafuta maji. Hawezi hata kuibeba mitungi wa maji. Mama ndiye atachukua punda wake mpaka mahali atakapopata maji. Wameumia ya kutosha. Kwa hivyo, inafaa tutafute namna ya kupata maji. Kama tungekuwa na maji, tungenyunyizia mashamba na tungekuwa na chakula kingi. Tungekua na maji katika kaunti yangu, hatungeuliza Serikali itupatie msaada wa chakula. Watu wangekuwa na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}