GET /api/v0.1/hansard/entries/494983/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 494983,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/494983/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "maji wangekuza chakula chao. Kuna sehemu nyingine ambazo zina mchanga mzuri lakini hazina maji. Kwa hivyo, sheria, au njia yoyote, itafutwe kuhakikisha kuwa maji ya mvua yamezuiliwa kila mahali. Wakenya wote inafaa kupata maji. Wafugaji wakilia kuwa hawapati maji, watu wa Nairobi pia wanalia hawana maji. Ni kama hakuna mtu ambaye ana maji. Hapo mbeleni, tulikuwa tukisema kuwa Ukambani ndiko hakuna maji. Lakini sasa hivi, kila mtu anasema hana maji. Inafaa tutafute njia yoyote ile Wakenya wote wapate maji safi. Kwenye mabwawa ya kuzuilia maji ambayo bado yanatumika, unakuta maji yameharibika mpaka yamebadilika rangi, lakini watu bado wanayakunyua. Hawana njia nyingine na hii inasababisha magonjwa. Mara kunatokea ugonjwa wa maji, ugonjwa wa ng’ombe na hata ugonjwa wa maziwa. Hii inasababishwa na kunyua maji ambayo si safi. Ng’ombe, binadamu na pia wanyama wa msituni pia wanakunywa hayo maji. Ukame ukiingia, ndovu, punda milia, ng’ombe, mbuzi na binadamu wanang’ang’ania hayo maji. Yule ambaye ataingia mapema ndiye atapata maji. Mambo ya maji yanafaa kuangaliwa. Ninaunga mkono kuwa maswala ya maji yabaki katika Serikali kuu. Kaunti zimepewa kila kitu na sijui kama zitaweza kutimiza maswala hayo au la. Maji yanafaa kubaki katika Serikali kuu. Ninaunga mkono."
}