GET /api/v0.1/hansard/entries/495005/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 495005,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/495005/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Mumo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 808,
"legal_name": "Rose Museo Mumo",
"slug": "rose-museo-mumo"
},
"content": "Sehemu nyingi za nchi zina ukame na watu wengi wanaosumbuka ni akina mama. Ni kwa nini tunazungumza juu ya maji wakati Kenya bado inapata mvua na tunaweza kukusanya haya maji kwa njia mbalimbali? Ni kwa sababu labda mikakati iliyopo yakukusanya haya maji ndiyo imechangia kuweko ukosefu wa maji ya kunyunyizia mimea maji na kupatia wanyama maji. Hii ndiyo sababu ninasema Serikali inafaa kuhakikisha kwamba kila Mkenya ama kila mwananchi anapata maji safi ya kutumia. Inafaa Serikali iweke mikakati mizuri. Wakati mwingi shida inayochangia ukosefu wa maji ni kamati ambazo zinateuliwa wakati maji yamechimbwa. Kamati inapata mafunzo lakini baada ya miaka michache mashine za maji zinaharibika na hasiwezi kutengenezwa na watu wanakuwa na shida iliyokuwako hapo mwanzoni. Hili ni jambo la kusikitisha. Kwanza, kamati zingine ni fisadi kwa sababu zinauza maji na hakuna uwajibikaji, au pesa wanazouza maji hazionekani zimeenda wapi. Kwa hivyo,watu wanarudi mahali walipoanzia. Ningependekeza sheria iwekwe ili wanachama wengi wa kamati hizi wawe ni akina mama. Hii ni kwa sababu wanaume hawatumii maji mengi. Mwenye kuumia ni mama. Akina mama wanajua uchungu wakutafuta maji kutoka mbali. Ninakumbuka nilipoenda huko Makindu, Makueni nilimpata mama mmoja ambaye alikuwa amejifungua na alikuwa amekaa siku nne bila kupata maji ya kuoga. Mnajua jinsi mama anavyokuwa anapojifungua. Inafaa Serikali iangalie sana sehemu ambazo ni kame hasa sehemu za Ukambani ambazo hazina maji na tumeongea juu ya jambo hili sana. Pia, inafaa Serikali iangalie ni wapi itachimba maji. Kuna vidimbwi vya maji ambavyo vimechimbwa lakini inafaa tuangalie ni vipi tunaweza kupata maji nyumbani. Kweli kuna njia nyingi za kupata maji. Tunaweza kupata maji ya mvua inaponyesha kwa kuyakusanya katika matangi. Ningependekeza haya matangi yapeanwe kwa watu na walipie kama bili ya maji kila mwezi. Hii itawasaidia watu kukusanya maji na kila familia itakuwa na maji. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Mswada huu. Ningependa jambo hili la maji liangaliwe sana hasa katika bajeti ya Kenya. Inafaa kiwango kikubwa cha fedha za Kenya kitumike kumpatia mwananchi maji ili tatizo la maji lisuluhishwe kabisa. Ahasante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}