GET /api/v0.1/hansard/entries/496652/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 496652,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/496652/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nataka kuunga mkono Hoja hii na haswa kuwapongeza Mhe. Kajuju na timu yake kwa kazi nzuri ambayo wamefanya kwa kutuletea Ripoti hii ambayo imeonyesha kwa uwazi kuwa kuna umuhimu wa sisi kama Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAM) kuweza kuendelea na kuhakikisha kuwa uhusiano wetu umezidi kuleta manufaa kwa wananchi wa JAM. Mhe. Naibu Spika wa Muda, Afrika Mashariki ilianza kitambo, miaka ile ya mwanzo wakati tulikuwa na JAM. Sifa nyingi inakwenda sana kwenye Jumuiya ya Nchi za Ulaya ambayo ilikuja kuchukua mfano Afrika Mashariki na kuweza kwenda kutengeneza jumuiya yao. Wao walisonga mbele kwa yale yote tulikuwa tumeyatakia wakati huo; walisonga mbele wakaweza kupata hela ama sarafu moja ambayo wameweza kuifanyia kazi na kuwawezesha wananchi wao kufanya biashara. Vile vile, sisi kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki tulivunja muungano wetu pale mwanzo lakini sasa hivi muungano umekuja na umekuja na nguvu sana. Muungano huu wetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatakikana kuendelea kujengwa. Tumekuwa tukiujenga polepole, lakini vile vile nchi zingine zimekuwa na uwoga kuwa labda tukiendelea na Jumuiya hii tutaumiza wananchi wetu. Lakini ukweli ni kwamba wakati umefika wakuwa ubinafsi tuondoe. Nchi tofauti tofauti zitaona manufaa wakati tukiwa tumeungana ili sote tuweze kufanyabiashara tukiwa kama ndugu moja, na vile vile kuwawezesha wananchi wetu kuweza kupita kutoka nchi hadi nchi wakiwa wanaweza kurahisishiwa usafiri wao, pia kuweza kufanya shughuli zao bila wasiwasi wowote. Ripoti hii imeonyesha wazi ya kwamba tukisonga mbele umoja wetu ndio utakuwa nguvu yetu. Umoja wetu ndio utakaotuwezesha kupata manufaa, haswa kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}