GET /api/v0.1/hansard/entries/496653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 496653,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/496653/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "biashara. Sisi ambao tunatoka kwenye mpaka, tumeona matatizo mengi kwa muda mrefu kwasababu ya tofauti za hela ambazo tunazitumia. Vile vile kwa sababu ya tofauti za kibinafsi kwa sababu wananchi tofauti wamechukua muda kukubali kuwa Afrika Mashariki imeamua kusonga mbele tukiwa kitu kimoja. Ripoti yenyewe imeonyesha wazi kuwa hata sisi kama Wakenya itatubidi kugeuza Kipengele cha 231 cha Katiba ili tuweze kuwezesha Benki Kuu ambayo itasimamia Afrika Mashariki kuweza kuchukua majukumu yale ambayo yamekuwa yakisimamiwa na Benki Kuu ya hapa nchini na hata zile za nchi zingine, itawabidi waangalie sheria ili kuwezesha kufanikisha jambo hili. Serufi ambayo itatumika itatuwezesha kuwa sawasawa. Italeta usawa na kuwezesha mtu akitoka nchi moja kwenda nyingine ajue kuwa amepata haki yake kutegemea ile serufi itakuwa inatumika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuna maswala machache ambayo watu labda hawakuyafikiria lakini nafikiria ikifikia miaka hii 10 inavyozidi kuendelea, maswala haya mengi yatakuwa yameangaliwa haswa kujitambulisha kama wewe ni mwananchi wa upande gani. Nchi zingine kama Tanzania nimeona bado wako nyuma kidogo kwa kuwa wananchi wao hawawezi kujitambulisha kwa urahisi kwasababu hawajaweza kuwapatia vitambulisho. Hayo ndiyo maswala ambayo yatawawezesha watu kupita kwa urahisi na vile vile kuweza kufanya shughuli hizi zao, haswa za kibiashara, ili wananchi wetu waweze kupata manufaa. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, tumetembea nchi za madola nyingi. Tumetembea ulimwengu mzima. Kila mahali tukienda tunaangalia mfumo gani ambao unaweza kutufaa. Kusema ukweli, ukienda kwenye Jumuiya ya Ulaya unaona tofauti kubwa sana kama wenzangu walivyotangulia kusema, ile faida ambayo unaiona kule. Ukienda Afrika ya Magharibi vile vile utaona kuna tofauti kubwa sana kwasababu ya umoja wa ile jumuiya walionayo, haswa ECOWAS ambayo inawawezesha kufanya shughuli hizi. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, mengi yamesemwa na wenzangu. Mimi sina budi kuunga mkono yote yaliyosemwa, haswa kwa kupongeza Kamati hii kwa kazi nzuri waliofanya na pia kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu wa Kenya wakati huu akiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuweza kuhakikisha kuwa tumeweza kusonga mbele tukiwa kitu kimoja kama Afrika Mashariki. Asante sana."
}